BWANA YESU atukuzwe mpendwa. Karibu nikujuze Neno la MUNGU. Leo nazungumzia ndoa takatifu. Ndoa ni makubaliano rasmi matakatifu kati ya Mwanaume na Mwanamke kuishi pamoja kama mke na mume, kwa kuanza na utakatifu na kumaliza wakiwa watakatifu. Ndoa takatifu ni kati ya Mwanaume mtakatifu na Mwanamke mtakatifu watakapoamua kufunga ndoa takatifu katika MUNGU aliye Mtakatifu. MUNGU anasema; '' Kwa hiyo mtayashika maagizo yangu, na kuyafanya; mimi ndimi BWANA.-Walawi 22:31'' Ndoa ni agano takatifu la siku zote za kuishi kwa wawili hao. Ndoa takatifu inatakiwa iambatane na utakatifu. Ndoa takatifu inaanza na Wokovu wa BWANA YESU na kuishi kwa kulitii Neno la MUNGU. Yakobo 4:7 ''Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.'' Kuna ndoa zilianzia bar, wanandoa hao wanatakiwa watubu na kuanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu wa BWANA YESU. Kuna ndoa zilianzia vichakani, wanandoa hao wanatakiwa watubu na kuanza kuishi maisha matakatifu ya Wo...