Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu Hii lazima ikupe maswali kua Mungu anafananaje? Biblia inatupa majibu kua Mungu anafananaje. Yohana 4:24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli Biblia inasema Kua Mungu ni roho Hivo basi Mungu akisema tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwasura yetu basi hapo tunajua kua Mungu anamfanya mtu ambae ni roho na yeye Ila huyo mtu ambae ni Roho kuna dhumuni kuu aliloumbiwa Aliumbwa ili atawale, Mungu baada ya kuumba kila kitu akataka mtawala na huyo mtawala alitaka afanane nae Kwahio Mungu akamfanya mtu ambae ni Roho Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake Mwanaume na mwanamke...