Bwana asifiwe wapendwa, Karibu tujifunze neno la Mungu, Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. MWA. 1:3-4 SUV Huu mstari ukiuangalia kwa wepesi hutoona ujumbe mkubwa ulioko ndani yake. Leo napenda tuuchambue kwa undani zaidi. • Kabla ya hapo nataka tutambue vitu vifuatavyo:- 1-Mungu ni Roho na wanaomwabudu wanapaswa kumwabudu katika roho na kweli 2-Jambo lolote tunaloliona sasa hivi lilianzia katika ulimwengu wa kiroho. > Baada ya kujua hayo twende kwenye maandiko matakatifu Mungu alivosema iwe na nuru na ikawa. >Ukisoma vizuri utagundua nuru haikutokea maana ingetokea na tunavojua tabia ya mwanga ukiwasha taa sehemu yenye giza, giza lote linatoweka. >Tunaona Mungu anatenganisha kati ya nuru na giza Maana yake ni kwamba katika ulimwengu wa kiroho nuru ilionekana ila katika macho ya nyama yaani ulimwengu huu wa mwili nuru haikutokea. >Kwa imani Mungu alitenganisha nuru na giza inamaana nuru il...