Bwana asifiwe wapendwa,
Karibu tujifunze neno la Mungu,
Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
MWA. 1:3-4 SUV
Huu mstari ukiuangalia kwa wepesi hutoona ujumbe mkubwa ulioko ndani yake.
Leo napenda tuuchambue kwa undani zaidi.
• Kabla ya hapo nataka tutambue vitu vifuatavyo:-
1-Mungu ni Roho na wanaomwabudu wanapaswa kumwabudu katika roho na kweli
2-Jambo lolote tunaloliona sasa hivi lilianzia katika ulimwengu wa kiroho.
> Baada ya kujua hayo twende kwenye maandiko matakatifu Mungu alivosema iwe na nuru na ikawa.
>Ukisoma vizuri utagundua nuru haikutokea maana ingetokea na tunavojua tabia ya mwanga ukiwasha taa sehemu yenye giza, giza lote linatoweka.
>Tunaona Mungu anatenganisha kati ya nuru na giza
Maana yake ni kwamba katika ulimwengu wa kiroho nuru ilionekana ila katika macho ya nyama yaani ulimwengu huu wa mwili nuru haikutokea.
>Kwa imani Mungu alitenganisha nuru na giza inamaana nuru ilikua imefichwa na giza ila Mungu akaitoa huko.
• Ukiomba jambo kwa Mungu kwa imani limefanyika tayari unachotakiwa ni kutenganisha iko kitu unachoomba na hilo giza linalofanya usione hiyo baraka yako.
•Ukishukuru kabla haujapata kutamfanya Mungu akubariki zaidi alivokukusudia.
Jambo jingine lakujifunza hapo.
Ukimpokea Yesu upo kwenye nuru tayari cha kufanya ni kujitenganisha na mambo yote ya giza ikiwemo marafiki,tabia hata mazingira.
Kama bado hujampokea Yesu kua Bwana na Mwokozi wako fuata sala hii na kisha tafuta kanisa la kiroho uweze kukulia wokovu.
SALA YA TOBA
BWANA YESU,NAJA KWAKO (MIMI) KAMA NILIVYO,NIMETAMBUA YA KWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI.NIMETAMBUA YA KWAMBA NI WEWE TU UNAYEWEZA KUNISAMEHE NA KUNITAKASA.NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE. NAOMBA ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU,NA KULIANDIKA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE. NAYAKABIDHI MAISHA YANGU KWAKO,UNILINDE NA MWOVU SHETANI. NAJITOA KWAKO KUANZIA LEO/SASA,UNIFANYE KUWA KIUMBE KIPYA NA UNITUMIE KAMA UPENDAVYO. AHSANTE KWA KUNIKUBALI AMEN.
Contacts
Email:ste.bernard@yahoo.com
Phone no:0659447445
Comments
Post a Comment