NYARAKA ZA YEZEBELI Inaendeleaa.... Sasa napenda kuendelea pale nilipoishia kwenye hili somo letu, nataka niwekee msisitizo zaidi kwenye eneo la nyaraka Mathayo 2:4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? Herodi alisikia Yesu kazaliwa Ila hakujua kazaliwa wapi Ila kwasababu anaufahamu wa mambo ya kiroho Akakusanya makuhani Na waaandishi wa watu Akawauliza Kristo kazaliwa wapi? herodi alijua kama kristo kazaliwa lazima hata sehemu aliozaliwa lazima iwe imeandikwa kua atazaliwa wapi Maana anajua kila kitu lazima kiandikwe kabla hakijatimia Mathayo 2:5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Wakajibu wakasema bethlehemu kama ilivyoandikwa Kumbe walijua kabisa Yesu atakua bethelehemu kwasababu imeandikwa hivo Kazi moja wapo ya Yezebeli ni anahusika na nyaraka Ukiona wewe unapita katika hali ya umasikini ujue Yesebeli kuna barua ameandika juu yako k...