Kati ya vitu ambavyo Mungu hupendezwa navyo ni umoja •Umoja unamruhusu Mungu afanye kazi pamoja na wewe MWANZO 1:26 "MUNGU akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,na kwa sura yetu wakawatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na wanyama na nchi yote pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi" Kupitia huo mstari tunaona kabisa Mungu akisema na " tumfanye" ni dhahiri kua Mungu hakua peke yake Alikua MUNGU BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU. Kwahio Mungu mwenyewe alimuumba binadamu katika hali ya umoja. •Mungu anaheshimu umoja na tukishikamana na kukubaliana Mungu anakua pamoja nasi. Matendo 4:31-32 " Hata walipokwisha kumwomba Mungu mahali pale walipokusanyika pakatakaswa wote wakajaa Roho mtakatifu wakanena neno la Mungu kwa ujasiri Na jamii ya watu walioamini walikua na moyo mmoja na roho moja wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe bali walikua na vitu vyote shirika.