Bernard Steven B wana YESU atukuzwe wapendwa Napenda tujifunze jambo ambalo litaponya na kutueka huru Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa Basi usipitwe na maarifa haya. Tambua kua Mungu hasemi kitu kwa sababu kina ukweli bali neno lake ni kweli. Na pia biblia inasema utaijua kweli na kweli utakueka huru, kwahio anaetaka kua huru basi soma hili somo ujifunze jambo upate maarifa na ulitendee kazi. Nataka tujifunze kuhusu vita vya mkristo. Tunatambua kua vita vyetu si vya mwilini bali ni vya rohoni. Sentensi hio yawezekana umeisema sana kwa kinywa chako au umeisikia watu wakisema lakini usielewe wanamaanisha nini. Wengi tunatamka kwa kinywa kua vita vyetu ni vya rohoni lakini kiuhalisia unapigana vita hivo kimwili. Wengi tumekua tukikerwa kidogo tu unagomba kweli na unajibizana na mtu aliekukera afu unasema unapigana vita vyako kiroho. Mtu kakutukana una mjibu na wewe afu unasema vita vyako unapigana kiroho. Umesingiziwa uongo unalala...