Skip to main content

Posts

Showing posts from June 13, 2016

YEHOVA YIREH-BWANA ATAPATA

  BERNARD STEVEN B wana Yesu asifiwe, Leo napenda tujifunze kuhusu moja ya majina ya Mungu wetu huyu mkuu. Kuna umuhimu kuyajua majina haya ya Mungu maana utajua jinsi ya kuyatumia katika mazingira tofauti. Jina tutakalo liangalia leo ni YEHOVA YIREH ambalo linamaanisha Bwana atapata. Ukisoma Mwanzo 22 yote utaona jinsi ibrahim alivoambiwa amtoe mwana wake wa pekee na hakusita lakini alipofika sehemu ya kutolea sadaka Bwana akampatia mwana kondo amtoe kama sadaka. MWA. 22:14 Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana. Sijui mlima gani unaoupitia, Je unauhitaji? BWANA atapata hitaji lako akupe kama alivopata mwana kondo wa kumpa ibrahimu. MUNGU wetu hana upungufu wa chochote. Rafiki yako unaweza kumuomba hela na akasema akipata atakupa lakini huwezi kuweka matumaini kwake maana yeye mwenyewe anamtegema Mungu ampatie. Lakini Mungu hakosi chochote kila utakacho muomba katika jina la Yesu atakupatia. ...

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

Total Pageviews

Followers