![]() |
BERNARD STEVEN |
Bwana Yesu asifiwe,
Leo napenda tujifunze kuhusu moja ya majina ya Mungu wetu huyu mkuu.
Kuna umuhimu kuyajua majina haya ya Mungu maana utajua jinsi ya kuyatumia katika mazingira tofauti.
Jina tutakalo liangalia leo ni YEHOVA YIREH ambalo linamaanisha Bwana atapata.
Ukisoma Mwanzo 22 yote utaona jinsi ibrahim alivoambiwa amtoe mwana wake wa pekee na hakusita lakini alipofika sehemu ya kutolea sadaka Bwana akampatia mwana kondo amtoe kama sadaka.
MWA. 22:14
Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.
Sijui mlima gani unaoupitia,Je unauhitaji? BWANA atapata hitaji lako akupe kama alivopata mwana kondo wa kumpa ibrahimu.
MUNGU wetu hana upungufu wa chochote.
Rafiki yako unaweza kumuomba hela na akasema akipata atakupa lakini huwezi kuweka matumaini kwake maana yeye mwenyewe anamtegema Mungu ampatie.
Lakini Mungu hakosi chochote kila utakacho muomba katika jina la Yesu atakupatia.
Ebu jiulize hili swali
Kwanini ibrahimu hakusita kumtoa mwanawe wa pekee ambaye amemsubiria kwa mda mrefu.
MWA. 15:1-6 SUV
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Hakusita kwa sababu ya imani yake kwa Mungu,Maana kama Mungu alisema kwamba atambariki kupitia isaka na ijapokua alikua bado mzee na akapata mtoto kwahio alijua kua hakuna jambo linalomshinda Mungu.
Kuna mengi unataka Mungu akupatie lakini imani yako je, inauwezo kweli wa kumfanya Mungu akupatie hiko unachomuomba
Imani yako ndo itakufanya upate unachomuomba Yesu
WAEBRANIA 11:17-19
17 Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa,
akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa
akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;
18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,
19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Katika hayo mahitaji yako muite JEHOVA YIREH na BWANA atapata cha kukupatia usiangalie majaribu au mazingira unayopitia saivi hio ni njia tu ya kufikia ubadae wako.
Lakini muite kwa IMANI.
Tumia jina hili JEHOVA YIREH pale unapopitia katika hali ya uhitaji na MUNGU atajidhihirisha kwako kama MUNGU asiepungukiwa na lolote na haja ya moyo wako atakupatia.
Comments
Post a Comment