2 Wakorintho 10:4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) Biblia inasema silaha za vita vyetu si za mwili. Kwahio tujue mpaka hapo tupo kwenye vita Maana hatuwezi tukawa tunaongelea kuhusu maswala ya silaha za vita wakati hatuna vita Kwahio hapo nikukujulisha kua tupo kwenye vita. Lakini pia ni kukujulisha kua hio vita haitumii silaha unazozijua hizi za mwili Yani bunduki,mabomu nk Ila zinauwezo katika Mungu, Kwa tafsiri rahisi hizo silaha zimetengenezwa na Mungu Na kila silaha inauwezo wake Tunajua kuna bunduki ina uwezo wake Kuna short gun pia kuna sniper hizi zote ni silaha lakini zinauwezo tofauti Hivo nategemea kuona silaha hizi ambazo zina uwezo katika Mungu zinauweza wake Na kutokana huu mstari tunajulishwa hizo silaha zinauwezo kiasi kwamba zinaweza kuangusha ngome Ngome ni majumba yaliojengwa kwa ufasaha ambayo ukuta wake ni mgumu na ni imara sana sio rahisi uanguke Kwahio hizo silaha zinauwezo wa kuan...