B wana YESU asifiwe, N apenda leo tujifunze kuhusu malaika. U mesikia sana neno hili malaika, je unajua ni nani huyu malaika? B asi fuatana na mimi katika hili somo uweze kupata ufahamu wa malaika ni nani hasa. NINI MAANA YA MALAIKA? K wenye lugha ya kingereza malaika anaitwa "angel" ila hilo neno limetolewa kwenye neno la kigiriki linaloitwa " angelos" ambalo kwa tafsiri yake halisi ya kingereza ni " messenger" . Kutokana na tasfiri hio basi tukija kwenye lugha yetu tunaona kua lina maanisha " mjumbe" M jumbe ni yule ambaye amebeba ujumbe wako au wa kitu chochote, kwahio tunapata maana yake kua malaika ni mjumbe kwahio kwa lugha rahisi na nyepesi malaika wako ni yule aliyebeba ujumbe wako. Ukisoma biblia yako vizuri utaona kua popote malaika alitokea alikua na ujumbe wa mtu. KUTOKA 23:20-22 " Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Ji...