{ Sehemu ya Tatu } Nataka nimalizie kanuni nyingine baada ya kukupa kanuni nane, twende pamoja. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: kuamini kupokea toka kwa Mungu. WAEBRANIA 11:6 "Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao" MARKO 11:24 "Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu" �� Hii ni kanuni ambayo Mungu kajiwekea kwamba wewe unayemuomba ni lazima uombe kwa imani na kuamini kupokea toka kwake Mungu. Kwahiyo ukiingia kwenye maombi huku ukawa huamini kwamba hilo unalomuomba Mungu atalijibu au laa, ujue hatajibu hayo maombi yako kwasababu hujaomba kwa imani na kuamini kupokea majibu toka moyoni mwako. Unapoingia kwenye maombi usiangalie hali yako au mzingira yanayokuzunguka ya tatizo lako bali wewe muombe Mungu kwa Imani kabisa huku ukitarajia kupokea ...