Bwana Yesu asifiwe? Talaka ni mpango wa shetani kuhakikisha kuwa umeishi maisha ya kuishi peke yako ila kusudi la Mungu ni uishi na mke/mume wako. Baada ya Mungu kumuumba Adamu, aliutoa ubavu wake na kumuumbia mkewe Hawa na Mungu ataitwa mwanamke maana ametolewa kwa mwanamume. Mwanzo 2:24 " Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake akaambatana na mkewe nao wawili huwa mwili mmoja " Ndoa ilianzishwa na Mungu mwenyewe na hakuianza kwa kusudi la kutalakiana ila ni idumu milele kwani ni kifo pekee chenye ruhusa ya kuitenganisha ndoa. Ninajua nimekukumbusha mengi kwa ujumbe huu maana ulitalakiwa au kutalakiana ila naomba kukwambia huo haukuwa mpango wa Yehova Mungu wako. Wengi talaka zao huletwa na uasherati/ uzinzi, ulevi, utasa/ugumba, usingiziaji, kukataliwa na mavyaa/ bavyaa na hata kuyatii mashauri madhaifu ya mchungaji wako ambaye anaweza kuwa ni nabii/mwalimu wa uongo. Pia najua ninakukumbusha kuwa unaweza kuwa ulichangia kuvunja ndoa ya mtu ila leo na...