Bwana Yesu asifiwe?
Talaka ni mpango wa shetani kuhakikisha kuwa umeishi maisha ya kuishi peke yako ila kusudi la Mungu ni uishi na mke/mume wako.
Baada ya Mungu kumuumba Adamu, aliutoa ubavu wake na kumuumbia mkewe Hawa na Mungu ataitwa mwanamke maana ametolewa kwa mwanamume.
Mwanzo 2:24
" Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake akaambatana na mkewe nao wawili huwa mwili mmoja"
Ndoa ilianzishwa na Mungu mwenyewe na hakuianza kwa kusudi la kutalakiana ila ni idumu milele kwani ni kifo pekee chenye ruhusa ya kuitenganisha ndoa.
Ninajua nimekukumbusha mengi kwa ujumbe huu maana ulitalakiwa au kutalakiana ila naomba kukwambia huo haukuwa mpango wa Yehova Mungu wako.
Wengi talaka zao huletwa na uasherati/ uzinzi, ulevi, utasa/ugumba, usingiziaji, kukataliwa na mavyaa/ bavyaa na hata kuyatii mashauri madhaifu ya mchungaji wako ambaye anaweza kuwa ni nabii/mwalimu wa uongo.
Pia najua ninakukumbusha kuwa unaweza kuwa ulichangia kuvunja ndoa ya mtu ila leo nakushauri kwa jina la Yesu ukatubu dhambi hiyo.
Katika maombi nimekuwa nikikutana na watu tofauti wakitaka neno la kinywa la kinabii la kujua kama anayekuoa/ unayemuoa ndiye ubavu wako. Watu hawa huwa na imani yakwamba nitakacho mwambia ndio kweli ya Mungu na mtu huwa tayari hata nikisema siye ubavu waachane ila hapa panahitaji hekima ya Mungu.
Kuna mafidhuli majibwa mwitu wanaopotosha watu wa Mungu kwa kuzivunja ndoa za watu kwa kuchangia kutalakiana huku wakidanganya wametumwa na Yehova Mungu. Ndugu husimwache mkeo/mumeo kwa ushauri mbovu wa mtu yeyote kwani ni laana kwa Mungu na kama ulikuwa umemwacha mumeo/mkeo mrudie leo.
Lisikie Neno la Yehova Mungu wako leo, Mungu anataka umtii na kuokoka ili ukaupate uzima wa milele. Talaka in mpango wa shetani wa:Kuiba,kuharibu na kuyaua maisha yako.
Hakikisha ndoa yako umeianza na kuitanguliza Yehova na itadumu milele.
Hakikisha umeiheshimu ile ya mwenzako kwani mwanzilishi wake pia ni Mungu wa mbinguni na ndiye kiongozi wake.
Kama una masikio nisikie ninavyokwambia kutoka kwa Yehova Mungu wa Israeli.
Kama hujaokoka okoka sasa, Yesu Kristo yu njiani kulitwaa Kanisa lake.
Ubarikiwe na usambaze ujumbe huu kwa marafiki zako.
Comments
Post a Comment