![]() |
ISAYA 28:13
"Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......"
"Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......"
Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu
Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu
anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na
kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka
nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo.
HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI:
Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi
{ i } Ni kuomba
Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako.
{ ii } Ni Mungu kusikia maombi yako.
Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi.
{ iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako.
Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yako.
{ iv } Ni Mungu kukujibu.
Mungu akishamaliza kutafakari maombi yako hatua inayofuata ni yeye kuyajibu maombi hayo.
Naamini katika hatua hizi za maombi kupitia umenielewa.
Usije ukafikiri kwamba ukiomba tu Mungu atajibu maombi yako hapana ni
mpaka asikie kisha atafakari hayo maombi, kisha ndipo sasa akujibu
haleluyaaaa.
MATHAYO 7:7-8
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa;
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa;
Kuna vitu ambavyo vimejificha hutaweza kuvipata mpaka umevitafuta wewe
kwa njia ya maombi. Na kuna mambo yako maishani mwako ambayo yamefungwa
kwahiyo hayataweza kufunguliwa mpaka umebisha kwa Mungu kwa njia ya
maombi.
Sasa ngoja nikupitishe kwenye hizo kanuni chache,
KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA:
1 Muombaji sharti usiwe mwenye dhambi.
YOHANA 9:31
"Tunajua kwamba Mungu HAWASIKILIZI watu wenye Dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake" ( Tafsiri ya Habari Njema )
"Tunajua kwamba Mungu HAWASIKILIZI watu wenye Dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake" ( Tafsiri ya Habari Njema )
2 Muombaji sharti ukae ndani ya kristo Yesu.
YOHANA 15:7
"Ninyi MKIKAA Ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, Ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"
"Ninyi MKIKAA Ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, Ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"
3 Muombaji sharti Uombe kwa Bidii sana.
YAKOBO 5:17
"Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, AKAOMBA kwa BIDII mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita"
"Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, AKAOMBA kwa BIDII mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita"
MATENDO 12:5
"Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa LIKAMWOMBA Mungu kwa JUHUDI/BIDII kwa ajili yake"
"Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa LIKAMWOMBA Mungu kwa JUHUDI/BIDII kwa ajili yake"
Huwa ili Mungu ajibu maombi yako ni lazima aione bidii yako wakati unaomba, lakini ukiomba kwa ulegevu hawezi kukujibu.
➡ Kwa sasa hivi naishia hapa katika kanuni hizo ila baadae nitakueleza kanuni nyingine.
Mimi ni rafiki yako Mtumishi Samweli Kibiriti
Utanipata kwa simu namba 0765 867574 na tigo ni 0673 784197 namba zote ziko WhatsApp.
Mungu akubariki sana.
Asante sana kwa hatua hizi mhimu za maombi,kuna kitu nimepokea.
ReplyDeleteMungu akubariki sana.
Mungu akubariki sana pastor
DeleteUbarikiwe mtumishi
ReplyDeleteAmen,tumebarikiwa
ReplyDeleteAkika Ni kipindi kizuri Mungu akuinue zaid
ReplyDeleteNAOMBA kuunganishwa na group la whatsp 0629344312
ReplyDeleteAmeeni nimekuelewa sana nanimejifunza
ReplyDeleteNaomba kuunganishwa na group hili la whatsp
ReplyDeleteMUNGU akubarik pastor na kukuinua katika viwango vingne
ReplyDeleteNaomba kuungwa kwa group la kufundiaha neno la MUNGU 🙏🙏
ReplyDelete0787741086
DeleteHalo watu wote, jina langu ni Marvelyn Larry. Kwa muda mrefu, mume wangu alikuwa akiishi katika ghorofa nyingine kutokana na shinikizo la kazi na tulifurahi sana pamoja ingawa alikaa mbali nasi kwa miezi kadhaa. Sikujua mwenzangu wa kazi tayari alikuwa na uhusiano naye jambo ambalo lilimfanya mume wangu anipe talaka bila kutarajia. Nilijua kuna kitu kibaya kwa sababu hatukuwahi kupigana au kubishana kiasi hicho ili kumfanya aondoke. Nilikuwa na kiwewe na natafuta msaada wa kukabiliana na hali hiyo iliyonipeleka kwa DR DAWN kutokana na sifa walizomwagiwa na watu mtandaoni. Tulizungumza kwa kirefu na aliniambia kila kitu nilichohitaji kujua kuhusu kile kilichotokea na utaratibu unaofaa wa kurekebisha matatizo. Alitimiza ahadi zake na kumrudisha mume wangu kwangu na mchakato wa talaka ukafutwa. Sasa mume wangu amerudi nyumbani kwetu na tuna furaha pamoja. Inashangaza sana jinsi watu wanaweza kusaidia watu wengine wakati wanahitaji. Anaweza kukusaidia pia. Mtumie tu ujumbe kupitia WhatsApp: +2349046229159
ReplyDeleteBarua pepe: dawnacuna314@gmail.com