![]() |
BERNARD STEVEN |
Bwana YESU asifiwe,
Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO.
Nini maana ya Manung'uniko?
Naweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia.Mara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU.
Kabla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa.
Hivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU.
Hujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika,
tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda.
HASARA ZA MANUNG'UNIKO
- Kufa kiroho kabisa nikiwa na maanisha kutokuona upenyo katika maombi, uwepo wa MUNGU kupotea kwako, hata ukiombewa hupati majibu
- Kunung'unika kunamfanya MUNGU asikupe baraka alizokukusudia
- Kunung'unika kunamfanya MUNGU akuache kwenye hayo mateso unayopita nayo
- Kunung'unika kutafanya hadi uzao wako upitie adhabu kutokana na kunung'unika kwako
Ila yote ujue yanasababishwa na ukosefu wa imani, yani humuamini MUNGU ndio maana unanung'unika nakuona kua MUNGU amekuacha.
MUNGU hupendezwa na imani na hii ndio sababu moja kwa nini MUNGU anapendezwa na imani maana mtu mwenye imani hata siku moja hawezi kumnung'unikia MUNGU.
YOTE HAYA SIJAYATOA KICHWANI MWANGU BALI KWENYE NENO LA MUNGU KWA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU
Kwa uthibitisho soma HESABU 14-26:38
MUNGU akubariki na usisahau kushare post hii kwa wengine
Nimebarikiwa sana na fundisho hili....
ReplyDeleteNamtukuza Mungu kwa ajili yenu....
Mungu azidi kuwainua mfike viwango vya juu zaidi katika huduma hii.
Amen barikiwa Sana
ReplyDeleteAmen barikiwa Sana
ReplyDeleteAmeeen be blessed abundantly
ReplyDeleteMungu akubariki mtumishi Kwa kuponya wahitaji
ReplyDelete