1- LUKA 1:37 " Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu" Tambua kua hakuna kinachomshinda Yesu, jambo unaloona ni gumu mnoo kwa Mungu ni dogo sana. , 2- ISAYA 49:15 " Je mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyae, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe" Tambua hata kama unapitia magumu kivipi Mungu hajakusahau na kama alivowakumbuka wana wa israel atakukumbuka. 3- EZEKIEL 37:5 " Bwana Mungu aiambia mifupa hii maneno haya, tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi" Kama kuna chochote kimekufa kwenye maisha yako basi ujue kinaweza kufufuka maana kama Mungu aliweza kutia pumzi na kuipa uhai mifupa mikavu, basi hilo jambo unalosumbuka nalo ni dogo sana ndugu muamini Mungu atakuinua na kukufikisha ulipokusudiwa. 4- YOHANA 14:13 " Nanyi mkiniomba lolote kwa jina langu, hilo nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya mwana" Ni nafasi ya kipekee kila mkristo amepewa kua ...