Jifunze kuyafuata mapenzi ya Mungu na kuyakubali. Wakati mwingine mapenzi ya Mungu yanaweza kuwa machungu kwako. Lakini ukiyakubali na kutii ziko faida kubwa. Lakini pia ziko hasara kubwa kama utayadharau na kutokuyafuata mapenzi hayo ya Mungu. Ni rahisi kusema Baba yetu uliye mbinguni mapenzi yako yatimizwe! Lakini yakitimizwa hatuko tayari kuyapokea wala kuyakubali! Maana sisi tunataka kuyapokea yaliyo mazuri tuu au yale yanayoziburudisha nafsi zetu hata kama siyo mapenzi ya Mungu. Kuna wakati mwingine yanatokea mambo magumu katika maisha yetu nasi katika hali hizo tunajikuta tunamkosea sana Mungu. Bila kujua yamkini pia hayo ni mapenzi ya Mungu kwako. Ukiisoma vizuri Bibilia utagundua kuwa matatizo aliyoyapata Ayubu yalikuwa ni mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa! Mungu ndiye aliyemruhusu shetani na kumpa kibali cha kwenda kutwaa mali zote za Ayubu. Lakini tunaona hata katika adha hiyo bado Ayubu alimtukuza Mungu na hakumkosea Mungu. Tujifunze kumtukuza Mungu hata tupitapo katika nyaka...