Skip to main content

JIFUNZE KUTAFUTA MAPENZI YA MUNGU

Jifunze kuyafuata mapenzi ya Mungu na kuyakubali. Wakati mwingine mapenzi ya Mungu yanaweza kuwa machungu kwako. Lakini ukiyakubali na kutii ziko faida kubwa. Lakini pia ziko hasara kubwa kama utayadharau na kutokuyafuata mapenzi hayo ya Mungu.

Ni rahisi kusema Baba yetu uliye mbinguni mapenzi yako yatimizwe! Lakini yakitimizwa hatuko tayari kuyapokea wala kuyakubali!

Maana sisi tunataka kuyapokea yaliyo mazuri tuu au yale yanayoziburudisha nafsi zetu hata kama siyo mapenzi ya Mungu.

Kuna wakati mwingine yanatokea mambo magumu katika maisha yetu nasi katika hali hizo tunajikuta tunamkosea sana Mungu. Bila kujua yamkini pia hayo ni mapenzi ya Mungu kwako.

Ukiisoma vizuri Bibilia utagundua kuwa matatizo aliyoyapata Ayubu yalikuwa ni mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa! Mungu ndiye aliyemruhusu shetani na kumpa kibali cha kwenda kutwaa mali zote za Ayubu.

Lakini tunaona hata katika adha hiyo bado Ayubu alimtukuza Mungu na hakumkosea Mungu.

Tujifunze kumtukuza Mungu hata tupitapo katika nyakati ngumu.

Tujifunze kumuinua Mungu hata pale yatupatapo mabaya.

Stephano anapigwa mawe lakini bado hakumkosea Mungu zaidi ya kutamka kuwa anaziona mbingu na pia kuwaombea rehema wale waliomuua.

Wakristo wengi wamekuwa siyo wavumilivu pale wanapopatwa na shida. Kwani wamekuwa watu wakukata tamaa sana na hata wakati mwingine kuiacha imani kabisa na kwenda kwa waganga wa kienyeji!

Kumbe huwezi kujua ni Mungu anakujaribu ili aone upendo wako kwake niwa kiasi gani.

Maana Mungu aweza kuruhusu jambo fulani gumu kwako ili na wengine wajifunze kupitia wewe alafu siku ya mwisho wamtukuze Mungu pale utakapovuka salama na kwa ushindi.

Mapenzi ya Mungu yanaweza kuwa na maumivu wakati fulani lakini simama na Bwana tena kwa shukurani mwambie Mungu asante hata kwa hili.

Ayubu akasema tupokee mema tu kwa Bwana na mabaya tusipokee!? Hapa ndipo hekima ya Mungu inahitajika sana.

Barkiwa


Comments

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)

Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho. { Sehemu ya pili } Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: 4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.     YOHANA 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"    WAKOLOSAI 3;16 "Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"     YEREMIA 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize" Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na ku...

Total Pageviews

Followers