PETER MABULA B WANA YESU atukuzwe ndugu. K aribu tujifunze. Mithali 8:17 ''Nawapenda Wale Wanipendao, Na Wale Wanaonitafuta Kwa Bidii Wataniona.''. - M aombi ni njia ya mawasiliano kati ya MUNGU na watoto wake waliosafishwa kwa damu ya mwanawe wa pekee YESU KRISTO. - M aombi ndio mawasiliano kati yetu wanadamu na MUNGU Baba yetu. Ili uhusiano wetu na MUNGU uwe hai lazima tuwe waombaji. Zaburi 62:8. '' Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; MUNGU ndiye kimbilio letu. '' - M UNGU huongea na sisi kwa njia ya neno lake kupitia kusoma kwetu Biblia na huongea na sisi kupitia watumishi wake, na sisi tunaongea na MUNGU kwa njia ya maombi, hivyo ili uhusiano wetu na MUNGU uwepo lazima tuwe na muda wa maombi. - B WANA Anatutaka Tumtafute Kwa Maombi - Tumtafute Kwa Matoleo -Tumtafute Kwa Matendo Mema -Tumtafute MUNGU Kwa Kumtegemea Yeye Peke Yake. -Tuombe Kwa Jina La YESU KRISTO Pekee (Yohana 14:13-14, Nanyi mk...