Skip to main content

TUMTAFUTE MUNGU MAADAMU ANAPATIKANA

 
PETER MABULA

BWANA YESU atukuzwe ndugu.

Karibu tujifunze.

Mithali 8:17

 ''Nawapenda Wale Wanipendao, Na Wale Wanaonitafuta Kwa Bidii Wataniona.''.

-Maombi ni njia ya mawasiliano kati ya MUNGU na watoto wake waliosafishwa kwa damu ya mwanawe wa pekee YESU KRISTO.

 -Maombi ndio mawasiliano kati yetu wanadamu na MUNGU Baba yetu. Ili uhusiano wetu na MUNGU uwe hai lazima tuwe waombaji.

Zaburi 62:8.

'' Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; MUNGU ndiye kimbilio letu. ''

-MUNGU huongea na sisi kwa njia ya neno lake kupitia kusoma kwetu Biblia na huongea na sisi kupitia watumishi wake, na sisi tunaongea na MUNGU kwa njia ya maombi, hivyo ili uhusiano wetu na MUNGU uwepo lazima tuwe na muda wa maombi.
-BWANA Anatutaka Tumtafute Kwa Maombi
- Tumtafute Kwa Matoleo
-Tumtafute Kwa Matendo Mema
-Tumtafute MUNGU Kwa Kumtegemea Yeye Peke Yake.
-Tuombe Kwa Jina La YESU KRISTO Pekee

(Yohana 14:13-14, Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. )

-Kila mtu ana wajibu wa kumtafuta MUNGU kwa maombi

-Maombi ni maisha ya waenda mbinguni.

-Maombi ni mkono mrefu wa kupokea baraka kutoka kwa MUNGU.

Maombolezo 3:25 

"BWANA Ni Mwema Kwa Hao Wamngojeao, Kwa Hiyo Nafsi Imtafutayo.".

-Ndugu mtafute BWANA.
MAOMBI NI MAISHA YA WATEULE, NA ILI UFANYE VYEMA NI MUHIMU KUJUA HAYA.
1. Tumtafute MUNGU Hata Hivyo MUNGU Hawi Mbali Na Kila Mmoja

(Matendo 17:26-27

Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute MUNGU, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.).

2. Tumtafute MUNGU Kwa Imani

(Waebrania 11:6

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. ).

3. Tuombe, Tumtafute Na Tubishe Kwenye Ufalme Wake ili tupokee baraka

 (Mathayo 7:7

 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; ).

4. Mjue Kwanza MUNGU kwa kumcha na ukizingatia kumcha MUNGU hakika utakuwa unamjua.

 (Mithali 2:4-5

Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua MUNGU.).

5. Omba bila kukoma na uzimzimishe ROHO MTAKATIFU.

(1 Thesalonike 5:17-19 

ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU. Msimzimishe ROHO;)

MUNGU Ameahidi Kwamba Tutamuona Kama Tu Tukimtafuta Kwa Bidii

(Yeremia 29:13

Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. ).

Tumtafute BWANA Wa Mabwana Maadamu Anapatikana, Tumwite Maadamu Ya Karibu Ila Mtu Mbaya Aache Dhambi Na Arejee Kwa BWANA Naye Atamrehemu

(Isaya 55:6-7

 Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. ).

BWANA YESU Anatupenda Sana.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula +255714252292
mabula1986@gmail.com
 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)

Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho. { Sehemu ya pili } Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: 4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.     YOHANA 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"    WAKOLOSAI 3;16 "Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"     YEREMIA 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize" Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na ku...

Total Pageviews

Followers