2 TIMOTHEO 2:20-21 20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine ni vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida. 21 Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema. Nyumbani mwa BWANA kuna vyombo vingi sana, vyombo vya fedha,dhahabu,mbao,udongo na vingine vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Ili MUNGU akutumie kwa viwango lazima uwe chombo kisafi kilichotakaswa au kwa lugha nyingine kilichosafishwa. Kuna watu ambao wapo nyumbani mwa BWANA lakini wao ni vyombo vichafu na MUNGU hawezi kuvitumia. Nitumie mfano huu wa nyumba ya kawaida, mtu ambae ana nyumba yake hua na vyombo vya kila aina lakini ili mtu huyu atumie hivo vyombo lazima ahakikishe hivo vyombo ni visafi maana hawe...