Skip to main content

VYOMBO NYUMBANI MWA BWANA

2 TIMOTHEO 2:20-21
20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine ni vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
21 Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema.

Nyumbani mwa BWANA kuna vyombo vingi sana, vyombo vya fedha,dhahabu,mbao,udongo na vingine vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Ili MUNGU akutumie kwa viwango lazima uwe chombo kisafi kilichotakaswa au kwa lugha nyingine kilichosafishwa.
Kuna watu ambao wapo nyumbani mwa BWANA lakini wao ni vyombo vichafu na MUNGU hawezi kuvitumia.

Nitumie mfano huu wa nyumba ya kawaida, mtu ambae ana nyumba yake hua na vyombo vya kila aina lakini ili mtu huyu atumie hivo vyombo lazima ahakikishe hivo vyombo ni visafi maana hawezi kuvitumia vikiwa vichafu.
Nyumba ambayo ina vyombo vichafu hata wageni wakija hua wanaishusha hadhi hio nyumba au muhusika wa hio nyyumbani.
Watu wengi wameshusha thamani nyumba ya BWANA kwa kujichafua kwa kutenda dhambi huku wapo hemani mwa BWANA wanakua ni kama vyombo vichafu viletavyo aibu hemani kwa BWANA.

Unaitaji kua msafi ili MUNGU awezew kukutumia kwa viwango vya juu zaidi, utakatifu ndio njia pekee ya kua msafi na hakikisha unaoshwa na kutakaswa kwa damu ya YESU kila wakati.

MUNGU hawezi hata siku moja kuona umuhimu wako katika kumtumikia yeye kama huishi maisha matakatifu kwa maana unakua ni chombo kichafu na katika kutumika kwako unaleta uharibifu zaidi hemani mwa BWANA.
Kwa maana yeyote anaetumia chombo kichafu kwa matumizi sio vizuri kwa afya yake vivyo hivyo kwa habari ya rohoni wewe kama chombo hemani mwa BWANA ukitumika huku unajichanganya changanya na mambo ya dunia utawanajisi wale unao wahudumia.

Mpendwa wangu katika BWANA ninakusihi kua ishi maisha ya kitakatifu kwa nzia leo hii ili MUNGU akutumie kwa viwango vya juu.

Ubarikiwe sana na somo letu halijaishia hapo bali litaendelea kua karibu na blog yako pendwa na usisite kuwaambia wengine waingie kwenye blog hii kujifunza neno la MUNGU.

Comments

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)

Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho. { Sehemu ya pili } Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: 4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.     YOHANA 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"    WAKOLOSAI 3;16 "Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"     YEREMIA 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize" Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na ku...

Total Pageviews

Followers