Chakula ni miongoni mwa vitu vinavyofanya mtu aweze kuishi. Lakini chakula hichohicho kinaweza kukuondolea UFAHAMU na UHAI wako ndani yako na kukufanya upoteze mwelekeo kabisa katika maisha yako. Tuone mifano ifuatayo; 1. ESAU ( Mwanzo 25;29-34 ) - Hapa tunaona jinsi ambavyo chakula cha Yakobo kinamfanya Esau auze haki yake ya UZALIWA WA KWANZA haijalishi alikuwa anaijali vipi lakini chakula kinamfanya asiwe na ufahamu wa kulinda na kuijali haki yake ya uzaliwa wa kwanza inayobeba mstakabali mzima wa yeye, familia yake na hata kizazi chake mbele yake. Ndio maana watu wengi wakialikwa kwenye sherehe hata kama kuna mambo machafu yanafanyika na uovu mwingi, miziki ya kidunia inapigwa huko lakini atakwenda kwa sababu ya chakula ( ufahamu wake umetekwa na kile chakula cha sherehe hata kumfanya auze haki yake ya kuwa mwana maombi, mhubiri, mwimbaji n.k 2. ISAKA ( Mwanzo 27:11 -27 ) - Chakula kinamfanya Isaka apumbazike na kupoteza ufahamu wa kutambua janja ya yakobo. Anamuuliza maswali...