Skip to main content

MANENO MANNE(4) YANAYOWEZA KUKUZA IMANI YAKO

1-LUKA 1:37
"Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu"
Tambua kua hakuna kinachomshinda Yesu, jambo unaloona ni gumu mnoo kwa Mungu ni dogo sana.
,
2- ISAYA 49:15
  "Je mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyae, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe"
Tambua hata kama unapitia magumu kivipi Mungu hajakusahau na kama alivowakumbuka wana wa israel atakukumbuka.
3- EZEKIEL 37:5
    "Bwana Mungu aiambia mifupa hii maneno haya, tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi"
Kama kuna chochote kimekufa kwenye maisha yako basi ujue kinaweza kufufuka maana kama Mungu aliweza kutia pumzi na kuipa uhai mifupa mikavu, basi hilo jambo unalosumbuka nalo ni dogo sana ndugu muamini Mungu atakuinua na kukufikisha ulipokusudiwa.
4- YOHANA 14:13
    "Nanyi mkiniomba lolote kwa jina langu, hilo nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya mwana"
  Ni nafasi ya kipekee kila mkristo amepewa kua na uwezo wa kuomba jambo lolote kupitia jina la Yesu na atatufanyia.
Note
Yote haya unaweza kupata tu kama utamkiri Bwana Yesu kua mwokozi wa maisha yako.
Fuata sala hii kama unataka kumpokea Kristo awe Bwana na mwokozi wako, Kisha tafuta kanisa la kiroho ili uweze kukulia wokovu.
SALA YA TOBA
BWANA YESU,NAJA KWAKO (MIMI) KAMA NILIVYO,NIMETAMBUA YA KWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI.NIMETAMBUA YA KWAMBA NI WEWE TU UNAYEWEZA KUNISAMEHE NA KUNITAKASA.NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE. NAOMBA ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU,NA KULIANDIKA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE. NAYAKABIDHI MAISHA YANGU KWAKO,UNILINDE NA MWOVU SHETANI. NAJITOA KWAKO KUANZIA LEO/SASA,UNIFANYE KUWA KIUMBE KIPYA NA UNITUMIE KAMA UPENDAVYO. AHSANTE KWA KUNIKUBALI AMEN.
Contacts
Phone no: 0659447445
Email: ste.bernard@yahoo.com

Comments

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)

Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho. { Sehemu ya pili } Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: 4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.     YOHANA 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"    WAKOLOSAI 3;16 "Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"     YEREMIA 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize" Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na ku...

Total Pageviews

Followers