Bwana Yesu atukuzwe?
Dhambi ni tendo lenye mvuto mkubwa ambapo mtu anapoitenda moja huvuta kiu fulani na kumpelekea mtu yuyo huyo kuitenda dhambi nyingine.
Shetani ni mshawishi mkuu wa kukutumbukiza kwa dhambi moja kwenda nyingine kwani atakuchochea uibie rafiki yako leo na ukifaulu atakuja tena kesho akukumbushe jana akwambie uirudie dhambi ile ya jana maana hakuna mtu alikuona.
Wakati huo utakuwa unasikia sauti ndogo ya kukunong'onezea ikikwambia: "Enda uregeshe kile ulichoiba jana na usirudie kuiba tena leo" Sauti hii inaweza kuwa ni wazo kwa akili yako kisha ukiitii huwa umempendeza Mungu wa mbinguni.
Unapofanya uzinzi/ uasherati na mwenzako, dakika moja baada ya tendo utasikia sauti fulani ikikuhukumu na kukuuliza kwanini umefanya uovu huu? Sauti hii ndio iitwayo Roho wa Mungu inayokuhukumu ukifanya dhambi na inakutaka utubu na kuacha kabisa dhambi hiyo.
Leo Mungu kupitia Roho wake amenituma nikwambie kuwa kuna kitu cha mtu umechukua na unajua vizuri kuwa sio chako.
Kuna mke wa mtu una-push naye na huku unajua kuwa ni mali ya mtu, Mungu anasema uache na utubu atakusamehea.
Kazi hizi unazozifanya ni za kishetani bali Yesu hataki huzifanye ila anakutaka ubadilike leo.
Kuna mume wa mtu unaishi naye kimapenzi huku mkewe analia kwa shida na kukosa upendo, Mungu ameniambia uache tabia hiyo kisha utubu. Yesu Kristo alikuja duniani kuvunja dhambi kama hizi na anatutaka tuache kabisa uovu huu.
1Yohana 3:8b
"Kwa maana mwana wa Mungu alidhihirishwa ili kuzivunja kazi za shetani"
Mkatae shetani na hila zake za kukunasa na dhambi moja hadi nyingine na umwendee Bwana Yesu siku ya leo.
Mtu aliye na masikio asikie sauti ya Yehova Mungu wa mbinguni na kuitii sauti yake.
Ubarikiwe kwa kuyasoma makala haya pia kama haujamkabidhi Bwana Yesu maisha yako, hakikisha umefanya hivyo sasa.
Comments
Post a Comment