Skip to main content

KANUNI ZA MAOMBI SEHEMU YA TATU

{ Sehemu ya Tatu }
Nataka nimalizie kanuni nyingine baada ya kukupa kanuni nane, twende pamoja.
KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA:
       kuamini kupokea toka kwa Mungu.
WAEBRANIA 11:6 "Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao"
MARKO 11:24 "Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu"
�� Hii ni kanuni ambayo Mungu kajiwekea kwamba wewe unayemuomba ni lazima uombe kwa imani na kuamini kupokea toka kwake Mungu. Kwahiyo ukiingia kwenye maombi huku ukawa huamini kwamba hilo unalomuomba Mungu atalijibu au laa, ujue hatajibu hayo maombi yako kwasababu hujaomba kwa imani na kuamini kupokea majibu toka moyoni mwako.
Unapoingia kwenye maombi usiangalie hali yako au mzingira yanayokuzunguka ya tatizo lako bali wewe muombe Mungu kwa Imani kabisa huku ukitarajia kupokea majibu toka mbele zake Mungu ok sawa eeee.
�� Muombaji sharti uwe na Uhusiano mzuri na Ardhi unayoikanyaga.
Hii ni kanuni ya ajabu sana ambayo Mungu kajiwekea kwenye ambapo huwa ardhi inafuatilia maisha ya watu wote wanaotembea juu yake. Watu wengi hawafahamu kuwa ardhi inao uwezo wa kumruhusu Mungu ajibu maombi yao au kumzuia Mungu asijibu maombi yao.
Nataka ufahamu kwamba ardhi unayoikanyaga kila siku huwa inafuatilia uhusiano wako ulionao na hiyo ardhi kila siku kwa jinsi unavyoishi juu ya hiyo ardhi. Ufahamu kwamba wakati Mungu alipokuwa anaiumba ardhi huwa kuna kanuni ambazo Mungu kaziweka ndani ya ardhi ili kufuatilia maisha ya wanadamu wote wanaotembea juu yake na moja ya kanuni ambayo Mungu kaiweka kwenye ardhi ni hiyo ardhi kumruhusu Mungu ajibu au asijibu maombi yako kutokana na wewe unavyoishi juu ya hiyo ardhi. Kuna mambo ukiyafanya kwenye maisha yako huwa ardhi itakuwa kinyume na wewe na kumzuia Mungu asijibu baadhi ya maombi yako unayomuomba.
2NYAKTI 7:14-15 "Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa"
Neno nchi hapa ni ardhi yenye mipaka halali ya kisheria, kwahiyo tunaona kwamba baada ya watu wa Mungu kuomba toba kwenye ardhi na kuacha njia zao mbaya basi Mungu atasikia hayo maombi na kuiponya Ardhi, hii iko na maana kwamba ardhi inaweza kuumwa.
�� Pia tunaona kwamba Mungu akiiponya ardhi kutokana na maombi ya toba yaliyofanyika juu yake ni kwamba macho yake yatafumbuka na masikio yake yatasikiliza maombi ya hao watu waliopo juu ya hiyo ardhi.
Ninachotaka kusema ni kwamba unapokuwa huna Uhusiano mzuri na ardhi unayokanyaga juu yake inaweza kumzuia Mungu asijibu baadhi ya maombi yako unayomuomba.
Muda sio mrefu nitakuletea somo hili la ardhi ambapo nitaichambua siri ya ardhi na nitakuonyesha mambo ambayo ikiyatenda ardhi inakiwa kinyume na maisha yako pia nitakuonyesha baadhi ya mambo ambayo ardhi huwa huyafuatilia kwenye maisha ya mtu n.k
{ 11 } Muombaji sharti uambatanishe maombi yako na sadaka kwa Mungu.
MATENDO 10:1-4 "Palikuwa na mtu kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu SADAKA nyingi, na kumuomba Mungu daima......Akamwambia, Sala zako na Sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu"
�� Hii pia ni kanuni ambayo Mungu kaiweka ya mwanadamu kuambatanisha maombi na sadaka mbele za Mungu. Kwahiyo hakikisha kwamba unaunganisha maombi yako na sadaka mbele za Mungu.
{ 12 } Muombaji sharti uambatanishe maombi yako na shukrani kwa Mungu.
YOHANA 11:41-42 "Basi wakaliondoa lile jiwe, Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. ...."
�� Hapa tunamuona Bwana Yesu anafika kwenye kaburi la Lazaro na kumshukuru Mungu kwa kuwa anamsikia kila siku kisha akamuita Lazaro atoke nje.
Saa nyingine hebu nenda mbele za Mungu kwa maombi ya kumshukuru Mungu tu kwq muda mrefu halafu utaona jinsi atakavyo kujibu maombi yako. Unajua tatizo letu tumezoea kila siku ni kumpelekea Mungu shida na matatizo yetu na hatuna hata muda wa kufanya maombi ya kumshukuru. Nakushauri hata kama uko na matatizo kiasi gani tenga muda wa kufanya maombi ya kumshukuru Mungu na yeye atashughulika na matatizo yako.
Na hapa ndio nimefikia mwisho wa somo hili la kanuni anazoangalia Mungu ili ajibu maombi yako ziko nyingi ila nimefanikiwa kukushirikisha hizo kumi na mbili. Katika kitabu nitakachokiandaa cha somo hili nitaelezea kanuni nyingine na kuingia ndani zaidi sana, Ninachokuomba zifanyie kazi hizi kanuni zote ili Mungu ajibu kila maombi unayomuomba kila siku.
Kwa mawasiliano utanipata kwa simu 0765 867574 na tigo ni 0673 784197 Email ni Samwelikibiriti@gmail.com
Mimi ni rafiki yako Mtumishi Samweli Kibiriti
Mungu akubariki sana sana kwa kuwa pamoja nami katika darasa la somo hili.
Jiandae kwa masomo mengine nitakayokuletea. Mzidi kutombea sisi watumishi wenu tunaowalisha Neno la Mungu.
MWISHO! MWISHO AMEN

Comments

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)

Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho. { Sehemu ya pili } Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: 4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.     YOHANA 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"    WAKOLOSAI 3;16 "Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"     YEREMIA 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize" Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na ku...

Total Pageviews

Followers