Bwana YESU asifiwe,
Napenda leo tujifunze kuhusu malaika.
Umesikia sana neno hili malaika, je unajua ni nani huyu malaika?
Basi fuatana na mimi katika hili somo uweze kupata ufahamu wa malaika ni nani hasa.
Kutokana na tasfiri hio basi tukija kwenye lugha yetu tunaona kua lina maanisha "mjumbe"
Mjumbe ni yule ambaye amebeba ujumbe wako au wa kitu chochote, kwahio tunapata maana yake kua malaika ni mjumbe kwahio kwa lugha rahisi na nyepesi malaika wako ni yule aliyebeba ujumbe wako.
Ukisoma biblia yako vizuri utaona kua popote malaika alitokea alikua na ujumbe wa mtu.
Ambaye yuko mbele yako kama kiongozi wako wa kiroho ambae MUNGU kamueka mbele yako huyo ni malaika wako.
Ni mjumbe wako maana amebeba ujumbe wako toka kwa MUNGU.
Anaposema anamtuma malaika aende mbele zako anamaanisha atamtuma mtumishi wake aje mbele zako. Akuonyeshe, akufundishe neno la MUNGU ili ujue namna ya kukaa na MUNGU ili akufikishe kwenye kusudi.
MUNGU anazidi kuhimiza msikilizeni akimaanisha msikilize sana kiongozi wako wa kiroho tii kile anachokufundisha.
Napenda leo tujifunze kuhusu malaika.
Umesikia sana neno hili malaika, je unajua ni nani huyu malaika?
Basi fuatana na mimi katika hili somo uweze kupata ufahamu wa malaika ni nani hasa.
NINI MAANA YA MALAIKA?
Kwenye lugha ya kingereza malaika anaitwa "angel" ila hilo neno limetolewa kwenye neno la kigiriki linaloitwa "angelos" ambalo kwa tafsiri yake halisi ya kingereza ni "messenger".Kutokana na tasfiri hio basi tukija kwenye lugha yetu tunaona kua lina maanisha "mjumbe"
Mjumbe ni yule ambaye amebeba ujumbe wako au wa kitu chochote, kwahio tunapata maana yake kua malaika ni mjumbe kwahio kwa lugha rahisi na nyepesi malaika wako ni yule aliyebeba ujumbe wako.
Ukisoma biblia yako vizuri utaona kua popote malaika alitokea alikua na ujumbe wa mtu.
KUTOKA 23:20-22
"Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.
Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao."
Ni hivi kutokana na hilo neno ukiangalia ufunuo uliopo ndani yake ni hivi:-
- MCHUNGAJI
- MWALIMU
- MTUME
- NABII
- MUINJILISTI
Ambaye yuko mbele yako kama kiongozi wako wa kiroho ambae MUNGU kamueka mbele yako huyo ni malaika wako.
Ni mjumbe wako maana amebeba ujumbe wako toka kwa MUNGU.
Anaposema anamtuma malaika aende mbele zako anamaanisha atamtuma mtumishi wake aje mbele zako. Akuonyeshe, akufundishe neno la MUNGU ili ujue namna ya kukaa na MUNGU ili akufikishe kwenye kusudi.
MUNGU anazidi kuhimiza msikilizeni akimaanisha msikilize sana kiongozi wako wa kiroho tii kile anachokufundisha.
Comments
Post a Comment