Isaya 48:12
Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia.
Mstari huu tunaona situation Mungu akitaka attention ya mtu lakini anamuita kwa majina mawili
Jina la kwanza anamuita yakobo alafu anamuita israel
Utashangaa kujua kua Mungu mwenyewe alimbadilisha jina Yakobo kua Israel na akamwambia kwanzia leo hutoitwa kwa jina la yakobo
Mwanzo 32:28
Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Kwahio Mungu mwenyewe alisema kua hatoitwa tena yakobo
Hii inatuonyesha kua ujumbe huu anaoutoa yamkini umesababishwa na yakobo na israel
Au kwa tafsiri nyingine umesababishwa na tabia za kale za israel
Ikiwa na maana Yakobo tabia za ukale
Maana tafsiri ya neno jina ni tabia
Kwahio akimuita mtu kwa jina la zamani ina maana bado anaona kuna tabia za zamani bado zipo ndani ya huyo mtu.
Au niseme hivi kama israel amebadilishwa jina
Ukiitwa kwa jina la zamani unaweza kuitikia maana itakuchukua mda kuzoea jina jipya
Sasa tafsiri yake ni hii
Ukiamua kubadilika tabia kuna vitu vinaweza vikafanyika vikakufanya bado utende kama zamani
Hivo basi Mungu anasema haya kwa sababu ameona israel bado anasumbuliwa na tabia za zamani (yakobo)
Anaendelea kusema mimi ni wa kwanza na wa mwisho pia
Ina maana kama ni mstari ukienda kuangalia wa kwanza ni nani utamkuta Mungu
Ukienda kuangalia wa mwisho nako utamkuta
Kwahio Mungu anajua habari za mwanzo na anajua za mwisho pia
Ina maana kama ni maisha yako anayajua tokea mwanzo na hadi mwisho hata kama hujafika mwisho
Kwahio haijalishi utapitia mangapi hapo katikati lakini mwisho wake Mungu anaujua tayari
Comments
Post a Comment