2 Wakorintho 10:4
(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
Biblia inasema silaha za vita vyetu si za mwili.
Kwahio tujue mpaka hapo tupo kwenye vita
Maana hatuwezi tukawa tunaongelea kuhusu maswala ya silaha za vita wakati hatuna vita
Kwahio hapo nikukujulisha kua tupo kwenye vita.
Lakini pia ni kukujulisha kua hio vita haitumii silaha unazozijua hizi za mwili
Yani bunduki,mabomu nk
Ila zinauwezo katika Mungu,
Kwa tafsiri rahisi hizo silaha zimetengenezwa na Mungu
Na kila silaha inauwezo wake
Tunajua kuna bunduki ina uwezo wake
Kuna short gun pia kuna sniper hizi zote ni silaha lakini zinauwezo tofauti
Hivo nategemea kuona silaha hizi ambazo zina uwezo katika Mungu zinauweza wake
Na kutokana huu mstari tunajulishwa hizo silaha zinauwezo kiasi kwamba zinaweza kuangusha ngome
Ngome ni majumba yaliojengwa kwa ufasaha ambayo ukuta wake ni mgumu na ni imara sana sio rahisi uanguke
Kwahio hizo silaha zinauwezo wa kuangusha hata hizo ngome
Sasa kwa nini silaha za Mungu zinapewa nguvu ya kuangusha ngome
Kwani vita yetu ni ya kuangusha ngome au?
Na je hizo ngome zinatuzuia nini sisi mpaka tuanze kuziangusha?
2 Wakorintho 10:5
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo
Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka
Kumbe mawazo ndio ngome inayoongelewa hapa.
Kumbe mambo yote unayowaza ni ngome unakua umeiinua
Je unawaza nini?
Sasa tukisoma juu tutazani tunatakiwa kuangusha kila ngome lakini
je hadi mawazo mazuri tuyaangushe?
Au biblia inataka kutumbia nini?
Anaendelea kusema na kila kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu
Kumbe mawazo ambayo tunatakiwa kuyaangusha ni yale ambayo yanataka kujiinua juu ya elimu ya Mungu
Elimu ya Mungu inasema huo ugonjwa unapona
Mawazo yako yanakwambia kua huo ugonjwa hauponi ina maana hayo mawazo yanataka kujiinua juu ya elimu ya Mungu
Kwahio hayo ni ya kuangusha tu
Unajiona kua hupendwi unajihisi kua mnyonge
Wakati elimu ya Mungu inakutaka uwe hodari na Yesu anakupenda
Hayo mawazo ni ngome inayotakiwa kuangushwa
Sasa ukishaangusha hayo mawazo
Kuna tendo la kigaidi unatakiwa kulifanya
Nalo ni tendo la utekaji
Unajua fikra zako zinagombaniwa na pande mbili
Kwa shetani na kwa Mungu
Lazima utumie silaha za Mungu kuteka fikra zako
Ukiteka mtu ujue yuko chini ya uangalizi wako na atafanya yote unayomwambia
Kwahio lazima uteke fikra zako na kuziamuru zimtii Kristo
Tumia silaha za Mungu kuteka fikra zako zimtii Kristo
Vita kubwa mtu hua anapitia nayo ni ya kwenye mawazo
Kwa sababu mawazo hujenga ngome
Sasa ni kitu gani unawaza
Anza kuangusha kwanza mawazo mabaya
Alafu ziteke fikra zako zimtii Yesu

Comments
Post a Comment