Bernard Steven |
Bwana YESU atukuzwe wapendwa
Napenda tujifunze jambo ambalo litaponya na kutueka huru
Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
Basi usipitwe na maarifa haya.
Basi usipitwe na maarifa haya.
Tambua kua Mungu hasemi kitu kwa sababu kina ukweli bali neno lake ni kweli.
Na pia biblia inasema utaijua kweli na kweli utakueka huru, kwahio anaetaka kua huru basi soma hili somo ujifunze jambo upate maarifa na ulitendee kazi.
Na pia biblia inasema utaijua kweli na kweli utakueka huru, kwahio anaetaka kua huru basi soma hili somo ujifunze jambo upate maarifa na ulitendee kazi.
Nataka tujifunze kuhusu vita vya mkristo.
Tunatambua kua vita vyetu si vya mwilini bali ni vya rohoni.
Sentensi hio yawezekana umeisema sana kwa kinywa chako au umeisikia watu wakisema lakini usielewe wanamaanisha nini.
Sentensi hio yawezekana umeisema sana kwa kinywa chako au umeisikia watu wakisema lakini usielewe wanamaanisha nini.
Wengi tunatamka kwa kinywa kua vita vyetu ni vya rohoni lakini kiuhalisia unapigana vita hivo kimwili.
Wengi tumekua tukikerwa kidogo tu unagomba kweli na unajibizana na mtu aliekukera afu unasema unapigana vita vyako kiroho.
Mtu kakutukana una mjibu na wewe afu unasema vita vyako unapigana kiroho.
Umesingiziwa uongo unalalamika kwa kila mtu unasema wamekuonea afu unasema vita vyako vya kiroho
Hapana kabisa vita vya kiroho hatupigani namna hio.
Wakikusema,wakikutukana,wakikuonea ingia chumbani mwako piga goti tamka msamaha kwa hao watu muachie Bwana.
Wakikusema,wakikutukana,
Kama mtoto wako mtundu mkabithi Yesu ashuhulike na tabia yake hivo ndo tunaishi sisi tulio rohoni.
Ila pia inawezekana kweli unapigana vita kiroho lakini umevaa silaha chache za kwenda katika hio vita ya kiroho.
Waefeso 6:11"Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani."
Kuna silaha ambazo ukizivaa rohoni hio vita lazima ushinde
Silaha za Vita
Katika vita hivi vya kiroho tunaitaji silaha.
Sasa utauliza tunavaaje hizo silaha wakati vita ni rohoni.
Hata silaha zenyewe unazivaa kwa namna ya rohoni.
Unachotakiwa ni kujua ni namna gani unavoweza kuvaa silaha zote.
Sasa utauliza tunavaaje hizo silaha wakati vita ni rohoni.
Hata silaha zenyewe unazivaa kwa namna ya rohoni.
Unachotakiwa ni kujua ni namna gani unavoweza kuvaa silaha zote.
Silaha ndo kama zifuatazo
Waefeso 6:14-17"Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;"
1-MKANDA-KWELI
Mkanda siku zote unamfanya mtu kua huru bila vazi alilovaa kumsumbua
Hivyo kama Mkristo lazima avae mkanda ambao hutokana na kuishi katika kweli.
Ili uweze kua na hii silaha kama mwanajeshi wa Kristo tembea kwenye ukweli
Ili uweze kua na hii silaha kama mwanajeshi wa Kristo tembea kwenye ukweli
Yohana mtakatifu 8:32"tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru".
Kristo ndio kweli (Ukitembea na Kristo umetembea katika ukweli)
Tukiwa na kweli tutakua huru ndio sifa ya mkanda kukufanya uwe huru katika shughuli zako.
Yohana 17:17" Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli."
Mstari huu unaongelea kuhusu kutakaswa na kweli, afu pia inasema kweli ni neno na pia tunajua neno ndio Kristo mwenyewe.
YOHANA 1:1-3"Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika".
Huo mstari unamuongelea Kristo kua ndio neno
Yohana 14:6"Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."
Inathibitisha kua kweli yenyewe ndio Kristo
2-DIRII-HAKI
Wengi hujiuliza haki ni nini, biblia inaposema haki ina maanisha kitu gani?
Haki kwa tafsiri ya Biblia ni kutokua na aina yeyote ya
uovu wala dhambi au kwa lugha nyingine mtu asie tenda dhambi ndio
anahesabiwa kua ni haki.
Warumi 9:30 "Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani"
Tukisoma hapo juu iinatudhihirishia kua haki ni kitendo cha kutokua na dhambi
Maana tunajua Yesu alikufa msalabani ili sisi tulio na dhambi tusamehewe maovu na tuwe na haki mbele za Mungu.
Maana tunajua Yesu alikufa msalabani ili sisi tulio na dhambi tusamehewe maovu na tuwe na haki mbele za Mungu.
Zaburi 37:21"Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu"
Inatoa tofauti kati ya mwenye haki na asiye na haki
Mwenye haki hupenda kutenda mema bali asiye na haki hufanya matendo yote ya kuzulumu na yasio mema.
Mwenye haki hupenda kutenda mema bali asiye na haki hufanya matendo yote ya kuzulumu na yasio mema.
Mithali 21:21"Aandamaye haki na fadhili, Ataona uhai na haki na heshima".
Pia haki ina uzima wa milele bali asiye na haki hana uzima wa milele bali mauti
1Yohana 3:7 "Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki"
Siku zote atendaye haki atapata haki kwasababu anaenenda
katika mapenzi ya Mungu lazima Mungu amuonekani kwa namna ya kipekee.
Kwa sasa nitaishia hapa ila kwa sasa tafakari haya mkiyangojea maendelezo yatayokuja hivi karibuni,
ila tutambue kua hizi silaha huwezi kuzivaa kama hujamkabithi YESU maisha yako, ebu leo chukua uamuzi wakuokoka ili uweze kumfurahia huyu YESU wetu kwa pamoja.
SOMA SALA IFUATAYO KAMA UKO TAYARI KUOKOKA
BWANA YESU,NAJA KWAKO (MIMI) KAMA NILIVYO,NIMETAMBUA YA KWAMBA MIMI
NI MWENYE DHAMBI.NIMETAMBUA YA KWAMBA NI WEWE TU UNAYEWEZA KUNISAMEHE NA
KUNITAKASA.NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE. NAOMBA ULIFUTE JINA
LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU,NA KULIANDIKA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA
MILELE. NAYAKABIDHI MAISHA YANGU KWAKO,UNILINDE NA MWOVU SHETANI.
NAJITOA KWAKO KUANZIA LEO/SASA,UNIFANYE KUWA KIUMBE KIPYA NA UNITUMIE
KAMA UPENDAVYO. AHSANTE KWA KUNIKUBALI AMEN.
Contacts
Email:ste.bernard@yahoo.com
Phone no:0659447445
Comments
Post a Comment