Bwana asifiwe,
Kila mtu anapenda kufanikiwa, lakini tatizo limekua ni namna gani ambavyo mtu unaweza kufanikiwa.
Leo nmewaandalia njia tano ambazo wewe mkristo ukifuatilia lazima uone mafanikio.
Unatakiwa ujue mambo haya kwanza kabla hujafikiria jinsi ya kufanikiwa
1. KUISHI VIZURI NA MUNGU
" Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa."
Tunaona kabisa kua ambaye atafuata sheria za BWANA ndo atakaefankiwa kwa kila atendalo. Tusiwe watu wa mizaha wala tusifuate mashauri ya wasio haki pia tupende kutafakari neno la MUNGU na kufanya yale yote MUNGU ametuamuru tufanye.
2. KUISHI VIZURI NA WATU
" 14 Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye.
15 Sauli alipoona ya kwamba alitenda kwa busara sana, yeye alimwogopa.
16 Lakini Israeli wote na Yuda wakampenda Daudi; kwa kuwa alitoka na kuingia mbele yao"
Tunaona jinsi Daudi alivoishi na watu vizuri mpaka sauli akaogopa maana alijua atachukua ufalme, hivyo kuishi kwetu vizuri na watu kuna tupa nafasi nzuri ya kufanikiwa maana huwezi kujua huyo ambaye unasema adui yako leo hujui kesho anaweza kua wa msaada gani kwako.
3. MTUMIKIE MUNGU.
"11 Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha."
4. AMANI
" 6 Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao"
Pia tunaweza kuona jinsi amani ya ayubu ilivotoweka shetani ndo akapata mlango wa kumuingilia
AYUBU 3:26
"26 Mimi sioni raha, wala situlii, wala kupumzika; Lakini huja taabu"
5. IMANI
" 30 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."

- Ni mapenzi ya MUNGU kuona wewe unafanikiwa
3 YOHANA 1:2
"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kua na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo"
- Ni MUNGU pia anayekupa nguvu za kuweza kufanikiwa
KUMBUKUMBU LA TORATI 8:18
"Bali utamkumbuka BWANA ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo"Baada ya kufahamu hayo sasa basi tutakwenda kuona ni vitu gani ambavo vinaweza kumfanya mkristo afanikiwe kwa kupitia mifano halisi kwenye neno la MUNGU.
1. KUISHI VIZURI NA MUNGU
Jinsi utakavoishi na kumpendeza MUNGU ndivo MUNGU atakapo kukubariki na kukuongeza zaidi na zaidi.ZABURI 1:1
" Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa."
Tunaona kabisa kua ambaye atafuata sheria za BWANA ndo atakaefankiwa kwa kila atendalo. Tusiwe watu wa mizaha wala tusifuate mashauri ya wasio haki pia tupende kutafakari neno la MUNGU na kufanya yale yote MUNGU ametuamuru tufanye.
2. KUISHI VIZURI NA WATU
Watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwa sababu ya kua na mahusiano mabaya na jamii yao. Wengi hata maofisini hawapandishwi vyeo kwasababu ya kua na mahusiano mabaya na wafanyakazi wenzako.1 SAMWELI 18:14-16
" 14 Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye.
15 Sauli alipoona ya kwamba alitenda kwa busara sana, yeye alimwogopa.
16 Lakini Israeli wote na Yuda wakampenda Daudi; kwa kuwa alitoka na kuingia mbele yao"
Tunaona jinsi Daudi alivoishi na watu vizuri mpaka sauli akaogopa maana alijua atachukua ufalme, hivyo kuishi kwetu vizuri na watu kuna tupa nafasi nzuri ya kufanikiwa maana huwezi kujua huyo ambaye unasema adui yako leo hujui kesho anaweza kua wa msaada gani kwako.
3. MTUMIKIE MUNGU.
Pia unaweza kufanikiwa kwa kumtumikia MUNGU kwa uaminifu. Unaweza kumtumikia MUNGU kwa njia tofuati, kuleta watu kwa YESU ni utumishi jitahidi kumtumikia MUNGU kwa njia hiyo ya kuleta watu kwake maana mtu mmoja akimpokea YESU huko mbinguni kunasherekea.AYUBU 36:11
"11 Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha."
4. AMANI
Amani ni muhimu mno, shetani ili aweze kupata mlango wa kukuingilia lazima avuruge amani yako, jitahidi ue na amani wakati wote usiruhusu huzuni moyoni mwako.ZABURI 122:6
" 6 Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao"
Pia tunaweza kuona jinsi amani ya ayubu ilivotoweka shetani ndo akapata mlango wa kumuingilia
AYUBU 3:26
"26 Mimi sioni raha, wala situlii, wala kupumzika; Lakini huja taabu"
5. IMANI
MATENDO YA MITUME 16:30Ukiwa ni mtu wa imani ziku zote utampendeza MUNGU, kwahio ukimuamini MUNGU kua anaweza kukufanikisha basi atakufanikisha.
" 30 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."
Comments
Post a Comment