![]() |
NYARAKA ZA YEZEBELI |
Inaendeleaa....
Sasa napenda kuendelea pale nilipoishia kwenye hili somo letu, nataka niwekee msisitizo zaidi kwenye eneo la nyaraka
Mathayo 2:4
Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
Herodi alisikia Yesu kazaliwa
Ila hakujua kazaliwa wapi
Ila kwasababu anaufahamu wa mambo ya kiroho
Akakusanya makuhani
Na waaandishi wa watu
Akawauliza Kristo kazaliwa wapi?
herodi alijua kama kristo kazaliwa lazima hata sehemu aliozaliwa lazima iwe imeandikwa kua atazaliwa wapi
Maana anajua kila kitu lazima kiandikwe kabla hakijatimia
Mathayo 2:5
Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
Wakajibu wakasema bethlehemu kama ilivyoandikwa
Kumbe walijua kabisa Yesu atakua bethelehemu kwasababu imeandikwa hivo
Kazi moja wapo ya Yezebeli ni anahusika na nyaraka
Ukiona wewe unapita katika hali ya umasikini ujue Yesebeli kuna barua ameandika juu yako kua wewe ni masikini
Kitu chochote shetani anachotaka kikutokee katika maisha yako lazima yezebeli akiandike kwanza
🌹Kwanini nasema yezebeli
Nitakupa mfano mwingine wa yezebeli alivoandika nyaraka
1 Wafalme 21:7-9
Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli.
Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia muhuri yake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi
Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu,
Alitaka nabothi auliwee
Kwahio kama kawaida yake alijua nguvu ya nyaraka
Na saivi akatumia jina la ahabu hakutumia jina lake
Inamaana shetani akitaka ufukuzwe kazi
Upewe barua ya termination
Yesebeli yeye ndo ataandika hio barua afu atatumia tu jina la boss wako
Kwahio unavopokea ile barua unazani ni boss wako kaandika kumbe ni roho ya yezebeli ilimvaa
Kwanini nyaraka zako muhimu hua zinakua shida kupatikana kwasababu roho ya yezebeli inazuilia hizo nyaraka
YESU ALIKUJA KUFUTA NYARAKA ZOTE ZILIZOANDIKWA JUU YAKO
Moja ya shughuli aliokuja kufanya Yesu ni kushughulikia nyaraka za YezebeliYesu alikuja kuifuta hati ilioandikwa
Na kuigongelea msalabani
Wakolosai 2:14
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
Kwahio moja ya kazi alizokuja kufanya Yesu ni kushughulikia vyote vilivoandikwa juu yetu na yesebeli ili visifanye kazi kwetu
Lakini usipokua na uelewa huo bado hizo nyaraka za yezebeli zitafanya kazi juu yako
ELIYA AMESHARUDI NA WAKAMFANYA VILE WALIVOANDIKA JUU YAKE
Wote tunajua elia alipaa mbinguni si ndo hivo
Na kati ya watu wa kwenye biblia unaweza kusema hawakufa unaweza kumtaja elia kama mmoja wao
Kwa namna hio unaweza kusema kwa kua eliya alipaa mbinguni basi nyaraka ya yezebeli haikufanya kazi
Lakini ebu tusome maandiko
Malaki 4:5
Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.
Katika kitabu cha malaki kinasema kua Mungu atamleta nabii eliya kabla siku ya Bwana
Biblia ikisema kabla siku ya Bwana ujue inamaanisha kabla ya Yesu
Kwahio eliya alitakiwa aje kabla ya Yesu
Swali je Eliya alikuja kabla ya Yesu?
Mathayo 17:11Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,
Yesu huyu akawaambia wanafunzi wake ni kweli kua eliya atakuja wa kwanza naye atatengeneza yote
Mathayo 17:12
ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
Akasema ila ameshakuja japo wengi hawajamtambua
Kama wengi leo ambavo hawajamtambua elia alivokuja
Mathayo 17:13
Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
Ndipo wanafunzi walipofahamu aah kumbe ni yohana mbatizaji
Kumbe eliya ndo yohana mbatizaji
Wakati malaika anamtokea zakaria baba yake yohana haya ndio maneno alimwambia
Luka 1:17
Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.
Yohana atatembea katika roho ya eliya
Inamaana eliya alikua katika mwili wa yohana
Anaeonekana kua ni Yohana mbatizaji agano jipya ndio eliya
Je kifo cha Yohana ni kama alivoandikiwa Eliya?
Mathayo 14:10
akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.
Ndio maana nyaraka ni muhimu
Nyaraka alioandikwa elia kua atauliwa kama alivowauw wale manabii 400
Maana aliwakata kichwa ndivyo alivouawa alivokuja kwa mwili wa yohana
Sasa kazi kwako kufuta na kuharibu kila nyaraka zote zilizoandikwa juu yako
🌹🌹Na nikwambie kitu yezebeli ni roho ambayo haijali unaupako kiasi gani
Kama yezebeli hakumuogopa eliya na ule upako wake wote hatukuogopa wewe kwa kukuandikia nyaraka
Na nisema tufurahi maana nyakati tulizopo ni za neema Yesu alishagongelea msumari nyaraka zote msalabani tumia nguvu ya msalaba kujipatia ushindi.
Ubarikiwe kwa somo hili.
Comments
Post a Comment