![]() | |
NYARAKA ZA YEZEBELI |
Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.
Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
neno nyaraka sio geni
Nyaraka ni documents
Documents zilizoandikwa jambo husika
Biblia ni nyaraka tofauti tofauti za watumishi wa Mungu zizlizoletwa pamoja
Nyaraka za yezebeli
Ni nyaraka au documents ambazo anaziandika yezebeli
Umuhimu wa nyaraka
Wewe unaweza kua dereva mzuri sanaNa traffick anaona kabisa unaendesha vizuri wala huendi kinyume na sheria za barabarani
Lakini akikusimamisha afu akagundua hauna driving license
Kwa kweli hapo hapo utapigwa fine
Ina maana documents ni muhimu sana
Nyaraka ni muhimu sana
Ni kutolee mfano wa kiroho
Yesu alipojaribiwa
Alimshinda shetani kwa nyaraka
Alikua anasema imeandikwa
Imeandikwa
Ina maana kama hayo alikua anasema Yesu yasingeandikwa Yesu asingeweza kuyatumia
Yesu kwa kutumia neno lililoandikwa
Au kwa kutumia nyaraka
Aliweza kumshinda Shetani
Sasa kuna nyaraka za Yezebeli
1 Wafalme 19:2
Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.
Huyu ni yezebeli kapeleka ujumbe kwa eliya
Baada ya eliya kuua manabii 400 wa baali kwa kuwakata vichwa
Yezebeli kamtumia mjumbe kua atamuua kama vile alivowauwa hao manabii
1 Wafalme 19:3
Naye ALIPOONA hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
Biblia inasema nae alipoona
Yani haijasema aliposikia
Inasema alipoona
Inamaana ujumbe uliletwa ulikua kwa maandishi
Ina maana yezebeli alimtuma mjumbe akampa barua inayosema hayo maneno
Sasa turudi nyuma taratibu
Kama yezebeli alitaka kumuua eliya kwanini alimtumia barua kwanza
Kwanini asinge mwambia yule mjumbe kamuue eliya?
Pili biblia inasema eliya alipoona hayo aliondoka kuhifadhi roho yake
Tujiulize nabii mkubwa kama eliya aliweza kuua manabii 400 yeye peke yake kwanini ametishwa na ujumbe unaotoka kwa mwanamke mmoja tu?
Kutokana na maswali hayo
Nataka nikujulishe kitu hichi siku ya leo
Kila kinachokutokea lazima kiwe kimeandikwa
Chochote unachopitia leo kimeandikwa mahali
Eliya alikimbia kwasababu alijua kitu kikishaandikwa lazima kitokee
Yeye kama nabii anajua nguvu ya maandishi anajua nguvu ya nyaraka
Wote tunajua eliya alipaa kwenda mbinguni
Ni kweli
Ila leo nitawaonyesha sehemu eliya anakatwa kichwa ili kutimiza yale yalioandikwa juu yake na Yezebeli
Marko 9:11
Wakamwuliza, wakisema, Mbona WAANDISHI hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
Wanafunzi wa Yesu wakamwuliza Yesu mbona waandishi
Soma vizuri inasema mbona waandishi
Hunena ya kwamba imempasa eliya kuja kwanza
Ilikua imeandikwa kua lazima eliya japo amepaa mbinguni lazima arudi tena
Sasa tutaona Yesu alichojibu
Marko 9:12
Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza upya yote; lakini, pamoja na haya, AMEANDIKIWAJE Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharauliwa?
Yesu akasema ni ukweli lazima eliya aje kwanza na kurejesa upya yote
Lakini akasema pamoja na hayo
Ameandikwaje mwana wa adamu
Kumbe hata mateso aliyopitia Yesu ni kwasababu ilikua imeandikwa
Lakini Yesu hakuishia kusema tu yale yalioandikwa juu yake
Marko 9:13
Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa.
Akasema eliya ameshakuja
Na wamemtenda yote kama alivyoandikiwa
Ina maana eliya yale aliyoandikiwa ndo wametenda
Na alichoandikiwa ni kua atauliwa kwa kukatwa shingo ama alivowakata wale manabii baali
Somo linaendelea na tutajua jinsi eliya alivorudi....
Mubarikiwe wote
Comments
Post a Comment