Skip to main content

TAFAKARI 6 ZA WATUMISHI WA MUNGU

Nabii Lightness Somi

"Ukiwa ni mtu wa kusikiliza utapotea,ukiwa ni mtu wa kusikia utafanikiwa"-LIGHTNESS SOMI

Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira

 "Tendo lolote baya, neno lolote baya na wazo lolote baya halina uhai. Kushindwa kwa mtu, kuharibiwa kwa mtu kuko katika mawazo yake. Chochote kibaya unachowaza au kusema au kutenda ni kwa ajili ya uharibifu wako, kushindwa kwako, kuangamia kwako na kifo chako.Kabla hujafanya jambo tafakari sana hilo wazo litaleta uharibifu au uhai wako? "-JOSEPHAT MWINGIRA

Mwl. Mwakasege
"Usifanye maombi ya kutaka kama vile"kumlazimisha" Mungu, ili akupe nje ya ratiba yake;kile alichokupangia ukipate, kufuatana na njozi aliyo nayo juu yako".- MWL. MWAKASEGE

Pastor. Chriss Oyakhilome
"Jaribu linaweza lisiondoke hata ukiomba, na lisipo ondoka ina maana Mungu anaamini amekufundisha vya kutosha kuweza kushinda hilo jaribu".-CHRISS OYAKHILOME
Prophet T.B Joshua
"Mtu mwenye malengo huangalia ubadae wake na sio mazingira, usiruhusu mazingira yakabadilisha mwelekeo wako"-T.B JOSHUA

Bernard Steven
"Siku zote mama mjamzito akikaribia kujifungua uchungu ndo unazidi, hata jaribu linapozidi kua kali tambua mwisho wake umekaribia, usikate tamaa, jipe moyo mkuu"-BERNARD STEVEN



Kama bado hujampokea YESU kua Bwana na mwokozi wako fuata sala hii kisha tafuta kanisa la kiroho uweze kukulia wokovu

SALA YA TOBA
BWANA YESU,NAJA KWAKO (MIMI) KAMA NILIVYO,NIMETAMBUA YA KWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI.NIMETAMBUA YA KWAMBA NI WEWE TU UNAYEWEZA KUNISAMEHE NA KUNITAKASA.NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE. NAOMBA ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU,NA KULIANDIKA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE. NAYAKABIDHI MAISHA YANGU KWAKO,UNILINDE NA MWOVU SHETANI. NAJITOA KWAKO KUANZIA LEO/SASA,UNIFANYE KUWA KIUMBE KIPYA NA UNITUMIE KAMA UPENDAVYO. AHSANTE KWA KUNIKUBALI AMEN.

Contacts
Email:ste.bernard@yahoo.com
Phone no:0659447445

Comments

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)

Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho. { Sehemu ya pili } Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: 4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.     YOHANA 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"    WAKOLOSAI 3;16 "Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"     YEREMIA 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize" Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na ku...

Total Pageviews

Followers