Skip to main content

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)


Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho.
{ Sehemu ya pili }
Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu.

KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA:

4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.
    YOHANA 15:7
"Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"
   WAKOLOSAI 3;16
"Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"
    YEREMIA 1:12
"Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize"

👉Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na kulitimiza. 
Kwahiyo hakikisha ndani ya moyo wako umelijaza Neno la Mungu na unapofanya maombi uyafanye katika msingi wa Neno la Mungu sawa.

5  Muombaji sharti uwaombee watu wengine.
       AYUBU 42:10
"Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo ALIPOWAOMBEA rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza"
Tafsiri ya Neno Biblia inasema  "Baada ya Ayubu KUWAOMBEA rafiki zake, BWANA akamfanikisha tena naye akampa mara mbili kama yale aliyokuwa nayo hapo kabla"
▶ Hapa Biblia inatueleza kwamba baada ya Ayubu kuwaombea kwa Mungu rafiki zake Mungu akageuza uteka wake na kumfanikisha mara mbili zaidi.

👉 Hii ni kanuni ambayo Mungu kaiweka na huwa anaifuatilia sana katika kujibu maombi ya watu kwamba je huwa wanawaombea watu wengine?. Sikiliza rafiki yangu ni lazima uwe kila   siku unatenga muda wa kuwaombea watu wengine wenye shida na matatizo mbalimbali usiwe mtu wa kujiombea tu wewe mwenyewe kwani Mungu asipokuona unawaombea watu wengine kuna maombi yako mengine hatakujibu hata kama utamuomba.

6 Muombaji sharti uombe kwa kutumia Jina la Yesu Kristo.
    YOHANA 14:13-14
"Nanyi mkiomba lo lote kwa JINA LANGU, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. MKINIOMBA neno lo lote kwa JINA langu, nitalifanya"
    YOHANA 16:23-24,26
"Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote, Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa Jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa JINA LANGU; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. Na siku ile mtaomba kwa JINA langu......."

👉 Hii ni kanuni ambayo Mungu kajiwekea kwamba maombi yote yanayoombwa kwake ni lazima mtu yoyote aombe kwa kutumia JINA la YESU KRISTO na sio kwa kutumia jina la Nabii au mtume au mchungaji au jina la Eliya au kutumia jina la bikra mariamu au mtakatifu yoyote yule. Ukiomba kwa kutumia jina lingine zaidi ya Jina la Yesu Kristo hayo maombi Mungu hatakujibu kabisa, umenielewa?

7 Muombaji sharti umpatie heshima Roho Mtakatifu katika maombi yako.
      WARUMI 8:26-27
"Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka. Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na Mapenzi ya Mungu" ( Tafsiri ya Habari Njema )
    YOHANA 14:26
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia"
➡ Wako watu wengi ambao wakitaka kuingia kwenye maombi huwa hawamshirikishi na kumpa heshima anayoshahiri Roho Mtakatifu. Huwa wao wanaona kwamba ni wataalam wa kuomba bila kujua kwamba Biblia imeweka wazi kabisa kwamba hakuna mtu anayejua kuomba ipasavyo na sawasawa na mapenzi ya Mungu bila msaada wa kuongozwa na Roho Mtakatifu.

👉 Nataka utambue kwamba Roho Mtakatifu ili akusaidie kuomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu nilazima utambue kwamba yuko na ametumwa duniani kutusaidia pia ni lazima umpe heshima yake,
              Ninaposema umpe heshima yake namaanisha nini? maana yake nikwamba kabla hujaanza kuomba mwambie "Roho Mtakatifu najua kwamba upo na umetumwa duniani kwaajili yangu nakuomba uniongoze katika haya maombi yangu na uniombee kama vile apendavyo Mungu sawasawa na mapenzi yake, karibu tuombe pamoja katika Jina la Yesu Kristo" Ukishatamka hivyo tayari Roho Mtakatifu anajua kuwa unaheshimu msaada wake na uko tayari akufundishe jinsi ya kuomba na kukuongoza na kukusaidia.

8 Muombaji sharti uwe mtii wa maagizo ya Neno la Mungu.
       ISAYA 1:19
"Kama mkikubali na KUTII mtakula mema ya nchi"

⚡ Kuna tofauti ya kukubali na kutii. Unaweza ukakubali Neno la Mungu( Biblia ) lakini usitii maagizo ya Neno la Mungu kwahiyo nilazima uikubali Biblia na vitabu vyake vyote kuanzia Mwanzo mpaka Ufunuo kisha uyatii maagizo yote ambayo Mungu ameyaelekeza ndani ya Neno lake ( Biblia )
    KUMBUKUMBU LA TORATI 28:1
"Itakuwa utakaposikia Sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa Bidii, kutunza kuyafanya Maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani"

👉 Hii ni kanuni ambayo Mungu kaiweka kwamba ili ajibu maombi yako nilazima aangalie Utiii ulionao katika Maagizo aliyoyaweka ndani ya Neno lake tumeelewana?. Hakikisha kwamba Unayatii maagizo yote ya Neno la Mungu hapo ndipo utamuona Mungu anayajibu maombi yako unayoomba.
⏩ Sasa kwa muda huu naomba niishie hapa katika kanuni hizi baadae nitamalizia kanuni nyingine ambazo Mungu amejiwekea ili aweze kujibu maombi ya wanadamu wanayomuomba.

👉 Naamini unazidi kubarikiwa na kanuni hizo, ninachokuomba endelea kutuombea watumishi tunaozidi kukuletea masomo mbalimbali ndani ya group hili ili Roho Mtakatifu azidi kutuongoza katika masomo ambayo Mungu amepanga tukufundishe.

➡ Kama utahitaji maombi au ushauri utanipata kwa mawasiliano haya simu 0765 867574 na tigo ni 0673 784197, kwa Email ni Samwelikibiriti@gmail.com
Mimi ni rafiki yako Mtumishi Samweli Kibiriti
Mungu akubariki kwa kujifunza somo hili

Comments

  1. Ubarikiwe sana Mwalimu

    ReplyDelete
  2. Naomba mniunge kwenye group hili la WhatsApp

    ReplyDelete
  3. Halo watu wote, jina langu ni Marvelyn Larry. Kwa muda mrefu, mume wangu alikuwa akiishi katika ghorofa nyingine kutokana na shinikizo la kazi na tulifurahi sana pamoja ingawa alikaa mbali nasi kwa miezi kadhaa. Sikujua mwenzangu wa kazi tayari alikuwa na uhusiano naye jambo ambalo lilimfanya mume wangu anipe talaka bila kutarajia. Nilijua kuna kitu kibaya kwa sababu hatukuwahi kupigana au kubishana kiasi hicho ili kumfanya aondoke. Nilikuwa na kiwewe na natafuta msaada wa kukabiliana na hali hiyo iliyonipeleka kwa DR DAWN kutokana na sifa walizomwagiwa na watu mtandaoni. Tulizungumza kwa kirefu na aliniambia kila kitu nilichohitaji kujua kuhusu kile kilichotokea na utaratibu unaofaa wa kurekebisha matatizo. Alitimiza ahadi zake na kumrudisha mume wangu kwangu na mchakato wa talaka ukafutwa. Sasa mume wangu amerudi nyumbani kwetu na tuna furaha pamoja. Inashangaza sana jinsi watu wanaweza kusaidia watu wengine wakati wanahitaji. Anaweza kukusaidia pia. Mtumie tu ujumbe kupitia WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Post a Comment

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

Total Pageviews

Followers