Bwana asifiwe wapendwa,
Unapoishi na wanadamu kukosana kupo,
Nikama glasi kwenye kabati zinazo kaa pamoja huwa hazikosi kugongana ...ndivo na binadamu wakaao pamoja amnavyo hawakosi kuhitilafiana
Pengine MUNGU ana maana yake ,wewe ukosewe,uachiliea MSAMAHA, ili nayeye akuchukue viwango fulani vya juu kwa sababu tu umetii agizo lake juu ya MSAMAHA.
KUSAMEHE NI AGIZO LA MUNGU
>Samehe saba Mara sabini
Luka 17: 4 " Na kama akakukosa Mara saba katika siku moja,na kurudi kwako Mara saba akisema nimetubu samehe.
>Ukisamehe utasamehewa
Mathayo 6;14-15
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao,na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao,wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
>Samehe kama ulivyosamehewa
Kumbuka waliotutangulia (Adam na Hawa) walivunja mzizi wa utii ,wakatuingiza kwenye mkumbo wa uovu.....
Warumi 3: 23-24
" kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa utukufu wa MUNGU
Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake,kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.
Waefeso 4:32
Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi,wenye huruma mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi"
TAFSIRI YA MSAMAHA HASA NI IPI ?
Kusamehe ni tendo la moyoni wala si kinywani au usoni linalokupa kujigharimu kurudisha mahusiano yaliyopotea
Kusamehe ni hali yakujishusha au kujinyenyekeza au kujitoa kwa gharama yoyote ile ili tu kuhakikisha umerudisha mahusiano yaliyopotea
Kurudisha mahusiano yaliyopotea siyo kazi rahisi. Unaweza ukakuta mwenzako anapanga kukuua, anapanga kuchoma moto nyumba yako,anapanga kukuchongea au kukusakizia balaa Fulani kwa sababu tu ya uhasama.
Akawa yeye nafsi yake imedhamiria kwa asilimia zote akufanyie baya . hakuongeleshi wala kukusalimia, akikuona barabara kuu yeye anakata uchochoroni, hataki hata kukuona wala
kukusikia.
Je UNAFIKIRI hapo mlipofikia nikazi rahisi?
Huwa inafikia hatua mahusiano kurudi yakahitaji gharama kubwa sana.
MSAMAHA siyo agizo la hiari bali ni agizo la lazima la MUNGU kwa mwanadamu. UKILIPUUZIA HUTOBAKI SALAMA
Kwa mfano. Unaweza kukuta mwingine alishakosana nawazazi wake na alishaapa hatokuja kuwasamehe wazazi wake hata iweje.
MUNGU anasema mtu wa namna hiyo hatabaki salama kupitia maandiko yake matakatifu
Mithali 20:20
"Amlaniye babaye au mamaye taa yake itazima katika Giza KUU"
WAEFESO 6:2-3
Waheshimu baba yako na mama yako,amri hii ndiyo ya kwanza yenye ahadi.
Upate heri ukae siku nyingi katika dunia
Kutoka 20:12
Waheshimu baba yako na mama yako ,siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA,Mungu wako .
"NIMEKUSAMEHE lakini SITAKUSAHAU"
Je,ungekuwa wewe ukasikia kauli hii kwa mshitaki wako utaipokeaje????
MUNGU atutie nguvu tukikutana tena tuiangalie kauli hii. Ukweli wake hasa ni upi
Ahsanteni
By
Silas Mayayz.
Comments
Post a Comment