Bwana Yesu asifiwe sana
Kichwa cha ujumbe huu nimekitoa kwa Biblia:
Mithali 7:18
"Nawapenda wanipendao na wenye kunitafuta kwa bidii wataniona".
Hii ni sauti ya Bwana Mungu akituelezea upendo wake kwetu.
Ni vigumu hata kwa maisha ya kibinadamu kumpenda asiyekupenda.
Ili upendwe ni lazima mwenyewe uwe unapenda kwa maana upendo haulazimishwi na uwezi kupendewa na mtu mwingine.
Ili Mungu akupende ni lazima uonyeshe dhana ya kumpenda kupitia njia tofauti.
Ili umpate Mungu ni lazima umtafute na sio kumtafuta pekee ila umtafute kwa bidii ndio umuone.
Kumbuka watu wanaomtafuta Mungu duniani ni wengi sana hivyo unahitajika kumtafuta kwa bidii sana ndio umpate.
Unapomtafuta Mungu ujue kuna mamilioni pia wanamtafuta Mungu yuyo huyo na na unahitajika utie bidii zaidi ili uwe wa kwanza kumuona.
Mungu mwenyewe ni Roho na ndio umuone ni lazima uwe na macho ya kiroho.
NJIA ZA KUMTAFUTA MUNGU WA MBINGUNI
Kuna njia tano za kumtafuta Mungu wa mbinguni ili umuone ndani ya maisha yako.Njia hizi ni:
1.Kutubu,kuacha dhambi na kuokoka.
2.Kuishi maisha ya maombi mengi ndani ya imani ya Bwana Yesu.
3.Kutoa sadaka/zaka/fungu la kumi.
4.Kumpa Mungu maisha yako yote kwa utumishi wa kazi take pasipo kutarajia chochote kama malipo.
5.Kulisoma na kulitii Neno la Mungu wa mbinguni huku ukienda ibada Kanisani.
Kama umekuwa ukimtafuta Mungu na bado haujamuona kwa kutimiza haya ujue unamtafuta Mungu ila haumtafuti kwa bidii.
Ndani yako tia bidii utaona mabadiliko baada ya kuutii ujumbe huu.
Watu wengi wanaenda Kanisani wakisema wanamtafuta Mungu na huku hawajasimamia wokovu.
Mungu anataka usimamie wokovu kwa ukweli.
Watu wengi wanatangaza mbinguni wao wenyewe wasioienda kwani wamejawa na unafiki huku wakisema wanamtafuta Mungu wa mbinguni.
Itakuwa ni aibu mpendwa mimi Geoffrey ninatumia muda mwingi nikihubiri injili nikose kuingia mbinguni huku niliowahubiria wakienda mbinguni.
Tubu dhambi zako leo mimi nimetubu zangu mpendwa tumtafute Mungu na tutamuona.
Ndio upone huo ugonjwa, hiyo hali mbaya ikuachie, wahitaji kutubu dhambi zako leo mpendwa kwa Bwana Yesu akuokoe.
Comments
Post a Comment