![]() |
BERNARD STEVEN |
Bwana YESU asifiwe,
Napenda kuendelea na mwendelezo wa somo letu la silaha za vita vya rohoni,
tumeshaangalia silaha mbili sasa leo naendelea na silaha ya tatu na kuendelea,
neno tunalo simamia ni:-
waefeso 6:14-17
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu
3-Kufungiwa utayari katika miguu
Miguu isiyokua tayari kwenda sehemu mwili huwezi kwenda, miguu ni sehemu muhimu kwa mwanadamu kwani mawazo huanza kwenye ufahamu lakini ili mawazo yako yatimie lazima uchukue hatua.vivyo hivyo sisi tuliofanyika wana wa MUNGU ni lazima tuwe na utayar wa kwenda kuhubiri injili kwa mataifa yani kwa wale wasiomjua YESU au wanamjua YESU lakini hawajui uweza wake.
MARKO 16:15
" Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe"
YESU katuamuru tuende kuihubiri injili kwa kila mtu ili waokoke.Una rafiki,ndugu,majirani ambao hawamjui YESU ebu chukua hatua nenda kawahubirie injili ya KRISTO.
Kua na utayari wa kutangaza injili ya YESU ni moja ya silaha za vita vya rohoni.
4-Imani-ngao
Kwenye vita ngao husaidia kujikinga na mishale hata na mapanga, ngao yako kama mkristo ni imani.WAEBRANIA 11:1
" Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."
Kupitia hapo tunajua kua imani ni kua na uhakika wa jambo ambalo liko mbele na hujaliona lakini una amini litakuwa.ila tutambue sio kila ila imani ni imani sahihi, imani sahihi na hakika ni ya kumuamini YESU
WARUMI 10:17
" Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo."
Na imani yenyewe ni moja tu,WAEFESO 4:5
" Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja."
Basi nikupe siri ya imani yako iweze kukua, huzuria ibada na mafundisho ya bible study na usome neno la Mungu
Kiasi cha neno la Mungu ndani yako ndio kiasi cha imani yako, huwezi kuamini zaidi ya ufahamu wako juu ya neno la Mungu.
5-Chapeo-wokovu
Wokovu ni kitendo cha kukombolewa kwenye dhambi na mauti yake.Wokovu unapatikana kwa YESU pekee nje ya hapo hamna wokovu.
Wokovu utakusaidia hata ukianguka kiroho uweze kurudi na kuanza safari na YESU.
chapeo ndio helmet yako inayokuzuia ukianguka uwe salama.
6-Upanga wa ROHO- Neno la MUNGU
WAEBRANIA 4:12
" Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo"
Neno la MUNGU lina nguvu na uwezo wa kujua mawazo ya mwanadamu, linauwezo wa kumbadilisha mwanadamu,linauwezo wa kumshinda shetani maana hata YESU alimshinda shetani kwa neno.Natumai umebarikiwa na somo hili la silaha za rohoni.Basi tusiwe wasikiaji wa neno tu bali watendaji, hapo ndo tutaona haya yote niliyo andika humu yakitenda kazi kwa kila mmoja wetu.
Somo zuri, kwa kuongezea kuna somo pia linaitwa VITA BADO VINAENDELEA...Kulisoma fuata link hii >>https://wingulamashahidi.org/2019/01/31/vita-bado-vinaendelea/...utaongeza maarifa...
ReplyDelete