Kutoka 3:2
Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
Yamkini una wito ndani yako na labda unajua kua Mungu amekuita kwa ajili ya kitu fulani.
Mungu akikuita ujue kuna maagizo anataka uyatekeleze, Mungu hatokuita tu ilimradi tu uokoke afu uwe unaenda kanisani na kurudi iishie hapo, kuna zaidi ya hapo, kuna kusudi maalumu kabisa ambalo anataka yeye alifanikishe hapa duniani na ili alifanikishe anaona ni vema akutumie wewe.
Wito sio kua mchungaji,mwalimu,nabii au mtume peke yake
Kazi yako inaweza ikawa wito wako pia.
Kupitia hio kazi Kuna vitu Mungu anataka kuvifanikisha hapa duniani.
Kuna hatua katika wito wako,zifuatazo ndio hatua za kuendea wito wako.
1- KUSHUHUDIA MATENDO MAKUU
Hatua ya kwanza katika Mungu kukutafuta wewe hua anakupa kibali cha wewe kushuhudia matendo makuu yakitendeka mbele ya macho yako,utaona watu wakiponywa,utaona miujiza ya kipekee ambayo hukuwahi kuzani vitu kama hivo vinaweza kutendeka, hii ni hatua ambayo Mungu alitumia kwa musa kwa kutumia kijiti kinachowaka moto bila kutekea huo ulikua ni muujiza unatendeka mbele ya macho yake na yote hio Mungu alifanya ili apate attention ya musa,Ni wengi sana wamemjua Mungu kutokana na kushudiwa na wao wenyewe kushuhudia matendo makuu ya Mungu yakitendeka ndio Mungu akapata attention yao hii ni kanuni anayotumia Mungu.
2- KUGEUKA
Kutoka 3:3
Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
Hatua ya pili ni kugeuka, dhumuni zima la Mungu kuweka muujiza ni ili kumfanya mtu amgeukie,
Musa aliegeuka akasema ebu nione kwanini hiki kijiti akiteketei, kwahio musa alikua anachunguza yawezekanaje kabisa kijiti hiki kisitekete wakati kinawaka moto, alikua ni mdadisi anatamani kuelewa. Hii ni hatua ya pili kwa mtu ambae Mungu humuita hua anadadisi sana miujiza na mda mwingine anataka kuhakikisha kama kweli hizo nguvu zatoka kwa Mungu au lah.
Ni hatu ambayo usipokua na neema ya Mungu unaweza ukaishia hapa hapa maana unaweza hata ukaona ni mazingaumbwe tu na hamna ukweli wowote.
3- KUITWA
Kutoka 3:4
Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
Mungu akishaona umegeuka na unajiuliza uliza maswali kuhusu mahali ulipo kama ni sahihi na miujiza inayotendeka, yeye mwenyewe atakuita kwa jina lako.
Umpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Siku yako ya kwanza kuokoka ilikua niwewe kuitikia katika sauti ya Mungu alikuita kwa jina lako.
Kuitikia ndio kumkubali awe Bwana wa maisha yako na akutawale hii ndio stage ya tatu
Na wengine huishia hapa pia maana huitwa lakini hawaitikii.
4- KUACHANA NA TABIA ZA UKALE
Kutoka 3:5
Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Baada ya Mungu kukuita hatua inayofuata ni Mungu anataka wewe uachane na tabia za ukale.
Tabia ulizokua nazo hapo mwanzo ulevi,uzinzi nk
Hivi vyote anataka uviache.
Kumbuka viatu vina ashiria utayari wako wa kwenda mahali.
Mungu alijua huyu Musa hatokubali ni kumtuma kwenda kwa wana waisrael kama hatovua viatu alivonavo saivi yani utayari aliokua nao wakati Mungu amekutana nae.
Kwahio Mungu anataka uachane na hizo tabia kwanza ili aweze kukutuma sasa kwa habari ya kazi.
Utashanga kugundua kua musa hakuvua viatu.
Kwasababu biblia nayotumia haionyeshi Musa akivua viatu
Kipengele hicho basi kinatupeleka kwenye hatua nyingine ya wito.
5- HOFU YA MUNGU
Kutoka 3:6
Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.
Baada ya Mungu kumwambia musa avue viatu alafu hakuona ushirikiano toka kwake, alichokifanya ni kujitambulisha kwake.
Mungu akianza kujifunua kwako akianza kukufundisha kuhusu yeye hii ni hatua ya kuelekea kujua wito wako.
Mungu akaanza kujitambulisha kwa musa kua yeye ni Mungu wa ibrahimu,isaka na yakobo kitendo hicho kilimfanya musa aogope.
Kumbe basi hofu ya Mungu huja pale unapomjua Mungu vizuri.
6- KUTUMWA
Kutoka 3:7Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao
Baada ya Mungu kujua sasa hakika una hofu ya Mungu ndani yako hapo ndipo Mungu sasa ataanza kujieleza kwanini alikuitwa atakwambia wito wako na utumishi ulioko ndani yako.
Kutokana na hatua hizi usitamani kuruka nenda kwa kanuni hizi na hautajichelewesha kwa kadiri unavotamani kumjua Mungu ndio hofu ya Mungu itazidi na ndipo utumishi wako utazidi kukua
Mwisho
Ubarikiwe kwa somo hili
Comments
Post a Comment