Skip to main content

WAMNGOJEAO BWANA

Isaya 40:31
bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Ebu vuta hisia zako uko mahali unamgojea mtu.

Afu jiulize unamgojea aje kufanya nini?

Je una appointment nae?

Kwa maswali haya tu ni dhahiri kabisa hauwezi kumngojea mtu kama hamjapanga mkutane mahali au kama hajakwambia umsubiri mahali.

Biblia inasema wamngojeao Bwana
Tujiulize kwanini unamgojea Bwana, je una appointment yeyote na yeye,
Je amekwambia umsubirie labda akuletee kitu.

Ebu tafakari unamgojea Bwana afanyaje?

Usije ukawa unamgojea wakati yeye hana taarifa yeyote kwamba unamgojea
Kwahio ili ufike hatua ya kumngojea mtu lazima pande zote mbili ziwe na taarifa
Yamkini kuna kitu umemuomba Mungu
Akasema subiri
Basi wewe unatakiwa umngojee Bwana.

Mungu akikuahidi jambo lazima ujifunze kumngojea hadi pale atakapotimiza

Ili uweze kumngojea Bwana

  • Anza kwa kumsikiliza yeye, jifunze kumsikiliza yeye
Kwa kumsikiliza huko huko ndo utapata maelekezo kua usubiri,
Sio vitu vyote ni vya kungojea vitu vingine Mungu anavifanya hapo kwa hapo kama ni wakati wake

Lakini vingine atakwambia subiri.
Utajuaje sasa kama amekwambia usubiri au lah.
Jifunze kumsikiliza.
Utajifunza kumsikiliza pale utakapokua msomaji mzuri wa neno na mtu wa kutafakari neno sana.

Neno linapokuja kwako, Mungu hulileta kama andiko na hua linabeba ujumbe ndani yake,
Huo ujumbe utaupata pale utakapoanza kutafakari hilo neno,
Huo ujumbe ndo kitu Mungu anachokusemesha.


Sasa ukishapokea huo ujumbe kama ni ahadi ya kitu atakachokutendea.
Jifunze kumngojea Bwana
Kumngojea ni kua na imani na kile ulichoahidiwa kua lazima kitimie hata ipite mda mrefu kiasi gani bado unaamini huko ndo kumngojea Bwana

Sasa faida za kuomngojea Bwana ni zifuatazo:

1- Utapata nguvu mpya
Kama kuna nguvu mpya basi ya zamani ipo, yamkini jana ulishinda misukosuko kwa sababu ya nguvu uliokua nayo jana
Haimaanishi hio nguvu inaweza kustahimili misukosuko yale
Hata wachezaje wa mpira au mchezo wowote hufanya mazoezi ili wapate nguvu mpya maana upinzani unafanya bidii kuongeza nguvu mpya kila siku

Nguvu mpya utaipata ukiwa na tabia ya kumngojea Bwana

Kwahio kumngojea Bwana ni kama mazoezi ya kuongeza nguvu
Zoezi la kumngojea Bwana litakupa nguvu mpya.

2-Watapanda juu kwa mbawa kama tai
Tabia ya kumngojea Bwana itakufanya ukue sana katika viwango kiroho na kimwili
Tai ni ndege ambae anaweza kuruka juu sanaa kuliko ndege wote.
Ina maana tabia ya kumngojea Bwana inakufanya uwe juu ya wote katika kila unachofanya

3-Watapiga mbio wala hawatachoka
Kumngojea Bwana kutakufanya uwe na speed.
Wengi huchokea njiani katika safari yao ya wokov, katika biashara zao maana wanaona walianza na mbio vizuri lakini sasa wamechoka hawaoni kwenda mbele
Kumngojea Bwana kutakupa kukimbia tu na utakimbia tu bila kuchoka

4-Watakwenda kwa miguu wala hawatazimia
Kutembea umbali mrefu kwa mda mrefu mda mwingine kutasababisha uzimie kwasababu ya kukosa nguvu
Lakini zoezi la kumngojea Bwana linakufanya uwe imara uweze kutembea umbali mrefu bila kuzimia
Nini maana ya kutembea,
Kutembea kuna ambatana na vile vitu unavofanya

Wagalatia 5:16
Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

Kuenenda kunaitaji miguu kwahio tunaposema kutembea bila kuzimia
Ni kutenda yale ya rohoni bila kuzimia yani bila kuacha.

Mungu akubariki kwa somo la leo

Comments

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

ZILIZOPENDWA ZAIDI

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

       ISAYA 28:13 "Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, KANUNI juu ya KANUNI, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo......" Mungu huwa anafanya kazi kwa kutumia kanuni zake alizojiwekea ili kuyaendesha maisha ya mwanadamu Kwahiyo unapofanya maombi ni lazima uelewe kanuni za Mungu anazotumia katika kujibu maombi ya wanadamu waliopo hapa duniani. Na kanuni hizo utazipata ndani ya Neno la Mungu, mimi kama mwalimu nataka nikusaidie kukuonyesha baadhi ya kanuni hizo. HATUA NNE ZA KUPITIA MAOMBI: Katika wewe kuomba huwa hayo maombi yako ni lazima yapitie ngazi/hatua hizi { i } Ni kuomba Nilazima wewe uombe hilo ni jukumu lako. { ii } Ni Mungu kusikia maombi yako. Unapoomba hatua inayofuata ni Mungu kusikia hayo maombi. { iii } Ni Mungu kutafakari hayo maombi yako. Baada ya wewe kuomba na Mungu kutafakari, huwa hatua inayofuata ni Mungu kuyatafakari hayo maombi yak...

HASARA ZA MANUNG'UNIKO

BERNARD STEVEN B wana YESU asifiwe,  Napenda tujifunze kuhusu manung'uniko na hasara zake kwa wewe MKRISTO. Nini maana ya Manung'uniko? N aweza kusema manun'guniko ni ile hali ya kulaumu au kulalamika kwa habari ya jambo fulani na kuona kua hustahili kupitia unayopitia. M ara nyingi mtu mwenye manung'uniko ni mtu ambaye hana shukrani mbele za MUNGU, mtu wa aina hii akipitishwa kwenye majaribu kidogo tu huoni kana kwamba MUNGU hayupo na anaweza hata kutoa maneno ya kufuru mbele za MUNGU. K abla hujaanza kunung'unika kwa habari ya hayo unayopita nayo, ebu jaribu kutafakari ulipotoka na ulipo sasa. H ivi unatambua kua hata pumzi uliokua nayo ni jambo la kusema asante kwa MUNGU. H ujajiuliza tu kwanini majaribu kwako hayaishi, basi tambua mengine si majaribu bali ni adhabu MUNGU ana achilia kwako kwa kunun'gunika, tambua kua wewe si wa kwanza kupitia majaribu, wapo wengi wamepitia na wameshinda. HASARA ZA MANUNG'UNIKO  Kufa kiroho kabisa ...

KANUNI ZA KUFANYA ILI MAOMBI YAKO YAJIBIWE NA MUNGU.(SEHEMU YA PILI)

Shalom rafiki yangu karibu sana tena leo katika somo letu hili la kupata maarifa ya kiroho. { Sehemu ya pili } Jana nilikuonyesha kanuni tatu nataka leo tuendelee na kanuni nyingine ambazo zitamfanya Mungu ajibu maombi yako, kwahiyo ni muhimu sana kuzifanyia kazi hizi kanuni kwasababu zitafanya maombi yako kujibiwa haraka na Mungu. KANUNI HIZO ZA KUMFANYA MUNGU AJIBU MAOMBI YAKO NI PAMOJA NA: 4 Muombaji sharti uliweke Neno la Mungu kwa wingi ndani ya moyo wako.     YOHANA 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO yangu yakikaa NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa"    WAKOLOSAI 3;16 "Neno la Kristo na likae au lidumu kwa wingi ndani yenu katika hekima yote"     YEREMIA 1:12 "Ndipo BWANA akaniambia, umeona vema; kwa maana ninaliangalia Neno langu, ili nilitimize" Maombi yanayoombwa kwa msingi wa Neno la Mungu huwa yanaleta majibu ya haraka kwasababu kanuni ya Mungu huwa ni kuliangalia Neno lake na ku...

Total Pageviews

Followers