Skip to main content

Posts

HATUA KATIKA WITO

Kutoka 3:2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Yamkini una wito ndani yako na labda unajua kua Mungu amekuita kwa ajili ya kitu fulani. Mungu akikuita ujue kuna maagizo anataka uyatekeleze, Mungu hatokuita tu ilimradi tu uokoke afu uwe unaenda kanisani na kurudi iishie hapo, kuna zaidi ya hapo, kuna kusudi maalumu kabisa ambalo anataka yeye alifanikishe hapa duniani na ili alifanikishe anaona ni vema akutumie wewe. Wito sio kua mchungaji,mwalimu,nabii au mtume peke yake Kazi yako inaweza ikawa wito wako pia. Kupitia hio kazi Kuna vitu Mungu anataka kuvifanikisha hapa duniani. Kuna hatua katika wito wako,zifuatazo ndio hatua za kuendea wito wako. 1- KUSHUHUDIA MATENDO MAKUU Hatua ya kwanza katika Mungu kukutafuta wewe hua anakupa kibali cha wewe kushuhudia matendo makuu yakitendeka mbele ya macho yako,utaona watu wakiponywa,utaona miujiza ya kip...

NYARAKA ZA YEZEBELI part 2

NYARAKA ZA YEZEBELI Inaendeleaa.... Sasa napenda kuendelea pale nilipoishia kwenye hili somo letu, nataka niwekee msisitizo zaidi kwenye eneo la nyaraka Mathayo 2:4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? Herodi alisikia Yesu kazaliwa Ila hakujua kazaliwa wapi Ila kwasababu anaufahamu wa mambo ya kiroho Akakusanya makuhani Na waaandishi wa watu Akawauliza Kristo kazaliwa wapi? herodi alijua kama kristo kazaliwa lazima hata sehemu aliozaliwa lazima iwe imeandikwa kua atazaliwa wapi Maana anajua kila kitu lazima kiandikwe kabla hakijatimia Mathayo 2:5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, Wakajibu wakasema bethlehemu kama ilivyoandikwa Kumbe walijua kabisa Yesu atakua bethelehemu kwasababu imeandikwa hivo Kazi moja wapo ya Yezebeli ni anahusika na nyaraka Ukiona wewe unapita katika hali ya umasikini ujue Yesebeli kuna barua ameandika juu yako k...

NYARAKA ZA YEZEBELI part 1

NYARAKA ZA YEZEBELI 1 Wafalme 19:2-3 Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko. neno nyaraka sio geni Nyaraka ni documents Documents zilizoandikwa jambo husika Biblia ni nyaraka tofauti tofauti za watumishi wa Mungu zizlizoletwa pamoja Nyaraka za yezebeli Ni nyaraka au documents ambazo anaziandika yezebeli Umuhimu wa nyaraka Wewe unaweza kua dereva mzuri sana Na traffick anaona kabisa unaendesha vizuri wala huendi kinyume na sheria za barabarani Lakini akikusimamisha afu akagundua hauna driving license Kwa kweli hapo hapo utapigwa fine Ina maana documents ni muhimu sana Nyaraka ni muhimu sana Ni kutolee mfano wa kiroho Yesu alipojaribiwa Alimshinda shetani kwa nyaraka Alikua anasema imeandikwa Imeandikwa Ina m...

GOD's ARMY APPLICATION FOR ANDROID USERS ONLY

Jipatie application ya GOD's ARMY kwa watumiaji wa simu za android pekee eg Samsung,Techno,Huawei,Sony,LG etc Kama unatumia Windows Phone,Iphone haitokubali DOWNLOAD HAPA

TOFAUTI YA ROHO NA MWILI

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu,kwa sura yetu Hii lazima ikupe maswali kua Mungu anafananaje? Biblia inatupa majibu kua Mungu anafananaje. Yohana 4:24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli Biblia inasema Kua Mungu ni roho Hivo basi Mungu akisema tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwasura yetu basi hapo tunajua kua Mungu anamfanya mtu ambae ni roho na yeye Ila huyo mtu ambae ni Roho kuna dhumuni kuu aliloumbiwa Aliumbwa ili atawale, Mungu baada ya kuumba kila kitu akataka mtawala na huyo mtawala alitaka afanane nae Kwahio Mungu akamfanya mtu ambae ni Roho Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake Mwanaume na mwanamke...

WAMNGOJEAO BWANA

Isaya 40:31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. Ebu vuta hisia zako uko mahali unamgojea mtu. Afu jiulize unamgojea aje kufanya nini? Je una appointment nae? Kwa maswali haya tu ni dhahiri kabisa hauwezi kumngojea mtu kama hamjapanga mkutane mahali au kama hajakwambia umsubiri mahali. Biblia inasema wamngojeao Bwana Tujiulize kwanini unamgojea Bwana, je una appointment yeyote na yeye, Je amekwambia umsubirie labda akuletee kitu. Ebu tafakari unamgojea Bwana afanyaje? Usije ukawa unamgojea wakati yeye hana taarifa yeyote kwamba unamgojea Kwahio ili ufike hatua ya kumngojea mtu lazima pande zote mbili ziwe na taarifa Yamkini kuna kitu umemuomba Mungu Akasema subiri Basi wewe unatakiwa umngojee Bwana. Mungu akikuahidi jambo lazima ujifunze kumngojea hadi pale atakapotimiza Ili uweze kumngojea Bwana Anza kwa kumsikiliza yeye, jifunze kumsikili...

NGOME YA KUANGUSHA

2 Wakorintho 10:4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) Biblia inasema silaha za vita vyetu si za mwili. Kwahio tujue mpaka hapo tupo kwenye vita Maana hatuwezi tukawa tunaongelea kuhusu maswala ya silaha za vita wakati hatuna vita Kwahio hapo nikukujulisha kua tupo kwenye vita. Lakini pia ni kukujulisha kua hio vita haitumii silaha unazozijua hizi za mwili Yani bunduki,mabomu nk Ila zinauwezo katika Mungu, Kwa tafsiri rahisi hizo silaha zimetengenezwa na Mungu Na kila silaha inauwezo wake Tunajua kuna bunduki ina uwezo wake Kuna short gun pia kuna sniper hizi zote ni silaha lakini zinauwezo tofauti Hivo nategemea kuona silaha hizi ambazo zina uwezo katika Mungu zinauweza wake Na kutokana huu mstari tunajulishwa hizo silaha zinauwezo kiasi kwamba zinaweza kuangusha ngome Ngome ni majumba yaliojengwa kwa ufasaha ambayo ukuta wake ni mgumu na ni imara sana sio rahisi uanguke Kwahio hizo silaha zinauwezo wa kuan...

Ni mfalme gani wa israel ambaye alifanya israel igawanyike na kua falme mbili?

Total Pageviews

Followers